Majibu yametolewa hapo juu na bwana Money stunna. Ni kwamba dola zimepungua hapa TZ kwasababu tunaangiza sana vitu nje Kwa kutumia dola na pia wahisani walisitisha kutoa dola zao kuisaidia TZ Kwasababu ya kashfa ya escrow. Kuhusu kununua vitu ebay, huko unalipa kwanza online Kwa kutumia credit card yako. Kuna maeneo ambayo bei inakuwa inajumuisha na gharama za utumaji wa mzigo. Kuhusu kodi ni kwamba mzigo wako ukishafika hapa utafikia mikononi wa TRA na utaukomboa huko Kwa kulipa kodi husika, kwahiyo bei inaongezeka.