Kwanini dollar inapanda namna hii kila kukicha?

Kwanini dollar inapanda namna hii kila kukicha?

The Only Kilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Posts
352
Reaction score
87
Wadau wa uchumi naomba mnipatie majibu yakinifu kwanini dollar inapanda sana kila hasubuhi.

Pia EXCHANGE RATE inafanyika je na nivigezo gani vinafuatiliwa kuandaa

Swali la nyongeza: Hivi ukinunua kitu online mfano ebay zile bei za bidhaa plus usafirishaji zinakutozwa bei mara mzigo ufikapo custom?? au nikishanunua ndo basi gharama haziongezeki tena?

Nashukuruni wote nikiwakumbusha kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kisha kupigia chama chako kura; usiwe tu shabiki wa chama flani halafu kesho na kesho kutwa unasema kura zinaibiwa wakati yako haipo hata bure.
 
Sababu kuna uaba aw dola, tunaagiza sana vitu Nje kuliko kuuza,ukumbuke wahisani walisitisha misaada kutokana na escrow.

pia kuna mabwanyenye uwa wanaficha dolla ili wauze kwa bei kubwa
 
sisi ni masikini watutegemezi, mahitaji yetu 90% tunaagiza kutoka nje.
 
Kutokana na sababu halo juu, sisi tunaihitaji sana dola ili kutimiza mahitaji Yetu ya kimanunuzi so tunaongeza demand ya dola, hivyo kuipaisha exchange rate (bei)
 
Majibu yametolewa hapo juu na bwana Money stunna. Ni kwamba dola zimepungua hapa TZ kwasababu tunaangiza sana vitu nje Kwa kutumia dola na pia wahisani walisitisha kutoa dola zao kuisaidia TZ Kwasababu ya kashfa ya escrow. Kuhusu kununua vitu ebay, huko unalipa kwanza online Kwa kutumia credit card yako. Kuna maeneo ambayo bei inakuwa inajumuisha na gharama za utumaji wa mzigo. Kuhusu kodi ni kwamba mzigo wako ukishafika hapa utafikia mikononi wa TRA na utaukomboa huko Kwa kulipa kodi husika, kwahiyo bei inaongezeka.
 
Back
Top Bottom