Hwa jamaa wanatumia nguvu sana kumnadi Kikwete! Ni kama wanamsindikiza askari mlemavu wa akili kwenda vitani! Pamoja na mbwe mbwe zote hawana imani maana upepo umegeuka sana. Nimepokea sms ikiwa na ujumbe wa kumkashfu Dr Slaa..... kama wengine kutoka "+3588108226" Nimepiga haipatikani nimetext sms haijawa delivered (Niweka matusi na kuwaambia sidanganyiki)
Kwa kweli Kinana na timu yake wanashangazwa!
Mwanakijiji,
CCM hawakutegemea Slaa kuwa mgombea wa CHADEMA (walihofia lakini hawakutegemea). Wao walijua mgombea atakuwa Baregu (au anayefanana naye - Mkumbo upooooo). Calculation zao zote zimekutana na surprise ambayo mpaka sasa wameshindwa wafanye nini kucounter wave yake.
Sina hakika sana na kitakachotokea Oct 31 ila nimejawa na hofu kubwa sana kwa nchi yangu.
Kama Dr. Slaa ataapishwa baada ya Tar 31 Oct Amin Amin nawaambia Watu wengi watatoroka hii nchi
Ukwepaji kodi na biashara haramu zinalindwaMwitikio wa CCM, makada wake na wapenzi wake dhidi ya Dr. Slaa umenishangaza sana. Toka alipotangazwa zimetumika mbinu mbalimbali za kumharibu kisiasa hata kibinafsi na nusura kidogo zifanikiwelakini zilipojibiwa kimahiri ikawa ni kama wao CCM wanamtengeneza shujaa mbele ya macho yetu. Ka nzi kalikopita sehemu mbalimbali mwishoni mwa juma kamejikuta kanashindwa kutoa taarifa ya sababu ya mwitikio huu.
Hata hivyo kanadokeza kuwa kati ya vitu vyote vinavyowatisha ni masuala ya EPA na Meremeta. Masuala haya mawili hawataki kabisa yaangukie chini ya mtu kama Dr. Slaa ambaye tayari amejionesha kuwa licha ya kwamba hana madaraka kuwatolea uvivu watuhumiwa wa uhalifu bila woga jambo ambalo limemshinda mtu aliyeko madarakani.
Lakini japo hilo linaelezea kutishwa kwa waliko madarakani lakini halitoshi kuelezea kutishwa kwa Chama kizima na kuwafanya wawe kama wanapigwa na ubaridi. Ninajiuliza kwa kadiri siku zinavyokwenda yawezekana watawala wakalazimika kuanza kutumia mbinu za wazi za vitisho kama walivyofanya miaka ile walipoanza kuonesha filamu za mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Lakini mbinu hiyo wameanza kuhisi haiwezi kufanikiwa kwani walitegemea wakihubiri juu ya umwagikaji damu basi watu wataanza kukwepa mikutano ya Slaa. Kinyume chake imekuwa kweli kwani watu wanachosema ni kuwa "hatudanganyiki".
Lakini ukweli bado unabakia kuwa kuna hofu ambayo haieleweki kwani siyo wana CCM tu bali hata taasisi nje ya CCM zinaanza kuonesha wazi kabisa kuhofia ajenda kali ya mabadiliko chini ya Dr. Slaa ambayo inavutia watu wengi zaidi (popular agenda).
Kilichowashangaza zaidi CCM kwa mujibu wa ka'nzi ni jinsi ambavyo wasomi (mijini) na wananchi wa vijijini wanavyokubaliana katika kumkubali Dr. Slaa. Huko nyuma watawala walitegemea utengano kati ya makundi hayo mawili huku baadhi ya kundi la wasomi likiiunga mkono CCM. Wanachofurahia hata hivyo ambayo inawapa matumaini kidogo ni kuwa bado CCM ni chama kinachokubaliwa na kupendwea na baadhi ya wafanya biashara ambao wanaamini katika chini ya CCM maslahi yao yanalindwa.
yangu macho...
Afichaye ugonjwa, kifo kinamuumbua!Kikwete alisema kuwa hayuko tayari ccm impasukie mikononi mwake,hivyo aliamua kuzinyamazia kashfa za ufisadi ilimradi chama kisonge mbele.Pia alisema hayuko tayari muungano uvunjike chini yake hivyo akawa mpole kutoa msimamo wake hata pale baraza la wawakilishi lilipopitisha miswada inayotia shaka,ilimradi kuwaridhisha.Kwa sasa hivi hayuko tayari ccm ipoteze dola chini yake hivyo atafanya afanyalo ilimradi dola ibaki kwa ccm bila kujali kuwa kwa ahadi nyingi anazotoa anakuwa anaichimbia ccm kaburi kwani iwapo ataingia madarakani hawezi zitekeleza,hivyo hakuna mtu ataichagua ccm tena 2015 hata za kuiba hawatazipata.Lakini hofu kubwa ni ukweli usiopingika kuwa Dk Slaa akiingia madarakani hakuna aliyefisadi nchi atakaye pona,hiyo ni pamoja na yeye JK.Mbali na hilo wamestushwa kuona jinsi umma ulivyomkubali Dk. Slaa.
Kwa namna hiyo basi nguvu nyingi za aina tofauti zitatumika ilimradi abakie madarakani.
Jana Mlimani TV walinikosha sana kwa kumuonyesha Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari pale Kilimanjaro Hotel mwaka 1995. Ukiisikiliza hiyo hotuba yake ama kuisoma kwenye kijitabu kinachoitwa NYUFA kwa kweli utaamini kwamba Mzee yule alikuwa anaona mbali na alikuwa mtabiri wa kweli wa hatma ya Tanzania si kama yule mzee wa majini pale Magomeni Mikumi! Mwalimu alisema Tanzania imeanza kuwa na nyufa kwa kukiuka misingi mizuri iliyokuwa imewekwa huko nyuma. Alizungumzia hatari za rushwa, ukabila na udini. Akasema nchi inanuka rushwa, Watanzania ni vulnerable ukabila haujaisha upo chini tu ya ngozi zao kwa hiyo usipoendelea kudhibitiwa ukabila utarudi. Akawaomba Watanzania wasiendekeze udini maana vyote hivyo ni hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi.
Mwalimu alizungumzia kwa kina kuhusu rushwa na jinsi inavyohitaji utashi na uongozi thabiti kushughulikia tatizo hilo. Akaeleza jinsi rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa kwa nguvu zote katika utawala wake. Wale waliokamatwa wakitoa ama kula rushwa walipelekwa mahakamani na walipohukumiwa Serikali ilikuwa imeishaweka adhabu ya kufungwa jela miaka 2 na kupigwa viboko 24! Mwalimu alitania kwamba hivyo viboko 12 mla rushwa/mtoa rushwa anapigwa anapoingia jela na 12 anapotoka jela akamuonyeshe mkewe! Akahadithia kwamba katika awamu yake aliwahi kukamatwa hata Mgiriki mmoja raia wa Cyprus corrupt mtoa rushwa ambaye alikuwa akitamba kwamba alikuwa ameiweka Serikali mfukoni. Alikamatwa, akapelekwa mahakamani, Akafungwa jela kama Watanzania wengine. Watu chungu nzima akiwemo Rais Kenyatta wa Kenya walijaribu kumuomba Mwalimu amuachie mgiriki yule, lakini Mwalimu akakataa kata-kata akisema mtu huyo ni mshenzi, alikuwa na mfuko mkubwa kiasi gani kuweza kuiweka Serikali yote mfukoni mwake?!! Hatimaye aliachiwa baada ya Askofu Mkuu Makarios wa Cyprus kutuma ujumbe kumuomba Mwalimu amsemehe mgiriki huyo. Mwalimu akakubali kwa masharti kwamba asionekane tena sio nchini tu bali Afrika Mashariki yote! Hivyo ndivyo rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa katika kipindi cha uongozi wa Mwalimu.
Sasa inavyoelekea Dr. Slaa ambaye ameonyesha dhahiri kuchukizwa na ufisadi ana mwelekeo wa kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere katika kurekebisha makosa kadha wa kadha yaliyofanywa na utawala wa CCM yanayohatarisha sana mstakabali wa Taifa letu. Kwa sababu hiyo lazima CCM waogope kwa kuwa endapo Dr. Slaa atafanikiwa itakuwa ni mwanzo wa mwisho wa mafisadi nchini mwetu!
Ushamuuza huyo mwandishi maana naamini Sumaye anamkumbuka ni nani aliyemhoji hapo private. lolWadau, hizi habari nazotaka kusema ni za kweli kabisa. Katika mahojianao miezi michache iliyopita, Frederick Sumaye aliwahi kumwambia mwandishi mmoja wa habari in confidence (na alimuomba hiyo iwe off record, yaani asichapishe) kwamba laiti JK angejua Slaa atachukuwa fomu za kugombea urais, basi yeye (JK) angejifikiria mara mia naye kuchukua fomu, na pengine asingechukuwa kabisa.
Wamejaribu kila aina za mbinu za kimafia ila wanashindwa na pia wataona kila kitu na kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja sasa