Elections 2010 Kwanini Dr. Slaa anawakosesha raha?

...Nitakuwa Airport kuhakikisha hakuna anayetoroka! maana ndicho kinachowasumbua.
 
Wasiojua wajue, na hata kama hawataki kujua walazimishwe kujua, na ccm pia wajue, kuwa chadema ipo juu na watu wanataka mabadiliko.


Ride Nutty Ride...... (bob Marley)
All now is a war, is fight against ruthless thieves
Who suck us blood
Like vampires!
To hell all !
 
DR SLAA ANAWAKOSESHA RAHA, NI KWELI

Sababu ni hizi

Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani. :smow:


Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini? :tonguez::A S 112:


Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.:decision:


Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious! :A S 13::moony:


Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu? :smow:


Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :hand:😛reggers:


Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.


Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..:smow:




[FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]​
 
Emancipate yourselves from entire slavery ,non but ourselves can free our minds
I have no fear for atomic energy,
Cause none of them can STOP The Time,
How long shall they kill our profits,
While we stand aside and look!
This is just a pot pit, we got to fulfill the pool!
Ts fire , fire , fire ! Right Nutty RIDE........

Mpaka kieleweke!
 
Nimetoka kuongea sasa hivi na mkuu mmoja ndani ya CHADEMA amedhibitisha kwamba wamesha dokezwa kwamba mtoto wa JK- Miraji ndie mwanzilishi wa some stupid sms. taarifa wametoa lakini hawategemei jipya. makanda wa CHADEMA wanajua hii ngoma refa ni mwananchi.
 
Naombi moja kwa makada wetu walioko Usalama wa taifa, tuendelee na uzalendo huo hata siku ya kuchokonoa kura wewe nenda hata ****** tupeni taarifa ili, pigeni hata picha mzitume tutawamaliza tu hao wezi.
 
Naombi moja kwa makada wetu walioko Usalama wa taifa, tuendelee na uzalendo huo hata siku ya kuchokonoa kura wewe nenda hata ****** tupeni taarifa ili, pigeni hata picha mzitume tutawamaliza tu hao wezi.

Hili ndo nawaomba wazalendo/makada wetu waliopo UwT, chukueni data, mkitumwa nendeni lakini dokezeni CHADEMA ili kutegua mtego wa hawa walafi wa madaraka!!

TZ bila CCM yawezekana! Chagua CHADEMA.
 

Haya mambo ni ya kutisha sana na si ya kupuuuza hata kidogo. Hii ina maana kwamba CCM inawatayarisha Watz kuipa amani na utulivu bye bye. Hivi CCM wanajua wanachokifanya?

Mimi nadhani ni kikundi kidogo tu cha wahindi -- kinachoipeleka nchi hii pabaya sana -- huku akina JK, Makamba, Kinana na wengine wakichekelea. Kukitokea sokomoko wote hawa watakimbia kwenda nje wakituacha wengine tukisagama humu ndani.
 

Makamba alituma mkwe wake (mke wa january) kwenda marekani kupata mtoto huko ili apate uraia wa marekani. Jamaa hawana uchungu kabisa na nchi yetu na mambo yakiharibika watakimbilia kwa wazungu.
 
Kelele zinazofanywa na mawaziri wanaomaliza muda wao zinatoklana na mashinikizo wanayopewa na viongozi wa CCM ambao hawapati usingizi, Kila wanakumbuka jina la Slaa basi wanapata nightmare za ajabu sana na kuanza kupiga simu huku na kule; mara Magufuri, mara kamala mara .................
 
acha wasilale kabisa maana siku zinazidi kumalizika....Byebye CHICHIEMu hahaha...
 
KAMALA baada ya kumwaga kwenye kura za maoni anajijua kuwa baada ya uchaguzi yeye atakuwa hana kazi kwahiyo
vigogo anavyorusha ni kwa ajili ya kutaka kufikiriwa ili angalau apewe cheo endapo bwana wake atashinda kwahiyo hana lolote
ni katika harakati zake za kutafuta ajira.
 



Kuna mmoja kaibuka leo ETI sera za elimu bure ni za sisiem, mbona walikua wanasema hazitekelezeki? ETI ni waziri!! nani kampa uwaziri wakati tuko kwenye mchakato wa kutafuta viongozi wa nchi? nadhani makatibu wakuu ndo wanapaswa kuendesha wizara AU? nirekebisheni
 
Very funny!!!!!! sihasa kweli si hasa. lakini jambio kweli jambio ni harufu yake kama inapendeza (ahh hili litamalizika tusi ngoja nibadili mkao) ni kuwa kama wapinzani wakilala basi CCM inayotawala italala na kama ikilalala maendeleo haytatakuwapo ni lazima Slaa amnyime usingizi kikwete kwa sababu ndiyo kazi yake kuwakosesha watu usingizi kama hafanyi hivyo hatakiwi kuwa huko.:bowl:
 

NDiyo maana Slaa anataka kubadilisha hii katiba isiyo na kichwa wala miguu!!!
 

Kamala ni chui wa kuchora, ashamwagwa na chama chake, wala hatishi. Marsha naye hio, hatishi. Mwaka huu wanang'oka tu.
 
You are very true mkuu PS ndo wanatakiwa waendeshe wizara kwa kipindi hiki, Ila hata mimi nimeshangazwa kusikia magembe eti kasema sera ya elimu bure ni ya ccm, what the heck!!!! wakati kila wanakopita wanasema sera hii ya chadema haitekelezeki, ni aibu na ni kutufanya wananchi hatuna akili, wajue siku hizi watu wameamka wanasimamia wanachoamini na wanachoona kuwa kinafaa, waache kudanganya wananchi si wote wajinga tuliozinduka ni wengi wakajipange upya wamepewa nafasi wameichezea sasa wakakamatane uchawi wao kwa wao. Tumechoka hatudanganyiki tena!! Mungu ibariki tz, mbariki Dr. Slaa,
 
Nimemsikiliza na kumsoma Kamala waziri wa EAC utetezi wake umekaa kipashkuna.Dr W Slaa ni mgombea urais wa JMT si Afrika mashariki.Mikataba ya kipuuzi kamwe haiwezi kuheshimiwa kwakuwa ilisainiwa na Kamala & Kikwete ,Rais ajaye ana kila sababu ya kuipitia upya kuangalia ina maslahi gani kwa wananchi wa Tanzania.

Dr Kamala kakataliwa jimboni kwake [alikozaliwa] baada ya kujua hana uwezo na ubunifu kuwawakilisha wananchi iweje leo atusemee watanzania zaidi ya milioni arobaini ?.
 

Nasikia jana Kamala ameambiwa asome gazeti la Gauradian, sikumbuki la tarehe ngapi. Laki Slaa akamwambia alisome kama anajua Kiingereza. Ina maana hajui Kiingereza? Ama kweli Dr. Slaa kamavalia njuga baada ya kumwambia mbumbumbu wa uchumi!

Kamala, KAA KIMYA COMRED.... ushauri wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…