Nadhan ulimaanisha engine+gearbox+diff kuwa mbele. Acha nijaribu kujibu kwa elimu yangu ya certificate..... Ili gari liwe na ufanisi barabarani inatakiwa upatikane msuguano wa kutosha kati ya tairi na ardhi ili 1. Gari liweze kusogea/kutembea 2. Gari iweze kusimama (brake) 3. Gari iweze kukata kona. Sasa mfumo wa engine mbele lengo ni kuweka uzito ili tairi ziweze kukamata ardhi sawasawa ili kupata ufanisi niliotaja hapo juu pia unaposhika brake 75% ya uzito wa gari unaenda mbele (weight transference) kama umefuatilia utagundua dereva anaposimamisha gari huwa linainamia mbele so ufanisi mzuri wa brake unategemea msuguano mzuri Kati ya tairi za mbele na ardhi
Sent using
Jamii Forums mobile app