Kwanini enzi na enzi wanyama hawa wamekuwa wakihusishwa na allegedly kushirikishwa katika uchawi/ushirikina.

Kwanini enzi na enzi wanyama hawa wamekuwa wakihusishwa na allegedly kushirikishwa katika uchawi/ushirikina.

Utakuta dini za kale za maeneo hayo ziliwapa uhusika mbaya,

Kwasababu ya maumbile yao au sifa flani.
 
Bututu ndio nini tena😂😂
images-7.jpg
images-6.jpg
 
FISI
MAMBA (Maeneo ya Ukerewe)
BUNDI
NYOKA
PAKA
NYUKI
PANYA


Ni siri gani hio ya kiroho inayounganisha viumbe hawa katika utekelezaji wa uchawi au ni stori tu za vijiwe vya gahawa?
ongeza na MBWEWA, SIMBA, TEMBO, CHUI na aina fulani za wadudu kama VUNJA CHUNGU hutumiwa sana baadhi ya maeneo kufanya uharibifu na kuleta madhara
 
Siku moja usiku wa manane paka walianza kulia usiku kwa uchuro Sana wife akataka kwenda kuwa vurumusha nikamkataza.

Kesho jion jirani yangu akafariki ghafla nyumbani kwake yaan we acha TU paka Wana vilio fulani Kama ana onewa dhurumiwa ni hatare
 
Baada ya Rais Kikwete atakuja Rais mweusi mchapa kazi, hata hivyo ataongoza kwa kipindi kifupi, ndipo Tanzania itapata Rais mwanamke na baada ya hapo Upinzani utachukua nchi,”… Sheikh Yahaya"
 
Baada ya Rais Kikwete atakuja Rais mweusi mchapa kazi, hata hivyo ataongoza kwa kipindi kifupi, ndipo Tanzania itapata Rais mwanamke na baada ya hapo Upinzani utachukua nchi,”… Sheikh Yahaya"
Hii ni DESTINY ngoja tuonee Ila Kuna wanao weza ku SKIP DESTINY ikasogezwa mbeleee...
 
Sanaaa mkuuu
Ndiyo maana niliwahi ng'atwa na nyuki nikaona si jambo la kawaida.

Iko hivi, mwaka 2021 mwezi wa tano, nikiwa natoka Kashishi (wilaya ya Kaliua) kwenda shule ya Sekondari Ilege (kupitia Kijiji cha Sasu), nilipokaribia kijiji cha Sasu, kulikuwa na kijipori flani hivi, ghafla niling'atwa mdomoni na nyuki maana kichwani nilikuwa na helmet.

Niliwashwa mwili mzima baada ya kung'atwa na nyuki. Kwa wenyeji wa kijiji hicho, ukiikamata njia ya kutoka Sasu kwenda shuleni Ilege, nilikimbiza pikipiki kwa kujikaza huku nawashwa lakini uvumilivu ulinishinda. Nilishuka kwenye pikipiki na kuanza kujikuna mwili mzima, hadi nilivua shati (hapo nipo njiani ila hakuna watu wengi).

Punde alitokea mzee akaniuliza nini kinanisibu, nilipomjibu kuwa nimeng'atwa na nyuki alicheka sana na kusema "nyuki wa Tabora wanakukaribisha mkoani kwao" kisha akasepa.

Nilijikuna baadae nikaona ujinga, nilitembeza pikipiki huku nawashwa ngozi yote ila nikasema sijikuni. Mpaka nafika shuleni, ngozi ilikuwa inawasha.

Kabla ya Kung'atw na nyuki huyo, nilizoea uking'atwa na nyuki utaumia eneo alilokung'ata pekee na baada ya hapo patavimba, lakini huyo akawa na utofauti huo.
 
Back
Top Bottom