Kwanini enzi na enzi wanyama hawa wamekuwa wakihusishwa na allegedly kushirikishwa katika uchawi/ushirikina.

Kwanini enzi na enzi wanyama hawa wamekuwa wakihusishwa na allegedly kushirikishwa katika uchawi/ushirikina.

Ndiyo maana niliwahi ng'atwa na nyuki nikaona si jambo la kawaida.

Iko hivi, mwaka 2021 mwezi wa tano, nikiwa natoka Kashishi (wilaya ya Kaliua) kwenda shule ya Sekondari Ilege (kupitia Kijiji cha Sasu), nilipokaribia kijiji cha Sasu, kulikuwa na kijipori flani hivi, ghafla niling'atwa mdomoni na nyuki maana kichwani nilikuwa na helmet.

Niliwashwa mwili mzima baada ya kung'atwa na nyuki. Kwa wenyeji wa kijiji hicho, ukiikamata njia ya kutoka Sasu kwenda shuleni Ilege, nilikimbiza pikipiki kwa kujikaza huku nawashwa lakini uvumilivu ulinishinda. Nilishuka kwenye pikipiki na kuanza kujikuna mwili mzima, hadi nilivua shati (hapo nipo njiani ila hakuna watu wengi).

Punde alitokea mzee akaniuliza nini kinanisibu, nilipomjibu kuwa nimeng'atwa na nyuki alicheka sana na kusema "nyuki wa Tabora wanakukaribisha mkoani kwao" kisha akasepa.

Nilijikuna baadae nikaona ujinga, nilitembeza pikipiki huku nawashwa ngozi yote ila nikasema sijikuni. Mpaka nafika shuleni, ngozi ilikuwa inawasha.

Kabla ya Kung'atw na nyuki huyo, nilizoea uking'atwa na nyuki utaumia eneo alilokung'ata pekee na baada ya hapo patavimba, lakini huyo akawa na utofauti huo.
Duh pole mkuu, ila uliponaje , dawa au iliisha yenyewe.
 
Baada ya Rais Kikwete atakuja Rais mweusi mchapa kazi, hata hivyo ataongoza kwa kipindi kifupi, ndipo Tanzania itapata Rais mwanamke na baada ya hapo Upinzani utachukua nchi,”… Sheikh Yahaya"
Hivi ni kwl alisema hivi au ni maneno ya watu
 
Baada ya Rais Kikwete atakuja Rais mweusi mchapa kazi, hata hivyo ataongoza kwa kipindi kifupi, ndipo Tanzania itapata Rais mwanamke na baada ya hapo Upinzani utachukua nchi,”… Sheikh Yahaya"
Utabiri ambao huwa hauoneshi tarehe wala mwaka gani ulisemwa au hata video yake ili tujue kama ni kweli Shkhe Yahya aliyanena hayo😄😄
 
Hii ni DESTINY ngoja tuonee Ila Kuna wanao weza ku SKIP DESTINY ikasogezwa mbeleee...
hii ya upinzani sio mwaka huu! mwaka huu ccm itashinda na kumalizia muhula wake.. hiyo ya upinzani ni 2030 toka kwenye chanzo kingine cha utabiri/watu wanaojua ulimwengu wa roho.

Tundu Lisu atakua na nguvu sana 2030 na inaweza kuwa ni Destiny yake! nikiangalia survival yake kwenye kuuwawa.. Mungu anataka kumpa zawadi!
 
TUNDU LISU ni VICTOR mtu mwingine angekua kesha kufa na kuoza kaburini
 
Huyu ndege anakula mizoga na ana uwezo mkubwa wa kunusa harufu ya mizoga. Zamani kulikuwa hakuna nyumba za kuhifadhia maiti hivyo watu wanapofariki walikuwa wanawekwa nyumbani. Harufu ilikuwa inavutia hawa ndege na kusogelea nyumba yenye msiba. Hili likafanya watu wahusishe huyu ndege na misiba. NB: kumbuka enzi hizo watu walikuwa wanaugulia nyumbani, hivyo wengine walikuwa wanatoa harufu hata kabla hawajafariki, jambo lililokuwa linavutia hawa ndege kwenda karibu na nyumba yenye mgonjwa. Wahenga walipoona dalili kama hiyo walijua msiba uko karibu.
 
😵‍💫😵‍💫😵‍💫
 
Duh pole mkuu, ila uliponaje , dawa au iliisha yenyewe.
Baada ya mzee yule kunicheka vile nimeelezea, hatua niliyochukua niliomba ombi lifuatalo;

"kama nimeng'atwa na nyuki wa kawaida, kusitokee chochote cha tofauti, muwasho uendelee. Kama ni nyuki aliyetumwa kwa hila, basi aliyemtuma maumivh nayoyapitia yamrudie mara mbili yake".

Baada ya kumaliza ombi hilo, kuna mmoja wa watu wa karibu ambaye tulikuwa hatujawasiliana kwa muda wa miaka miwili, alipiga simu. Baada ya kupokea na baada ya salamu akasema subiri kidogo nakupigia, hakupiga tena simu mpaka baada ya miezi sita.

Ndani ya nusu saa, maumivu yalikwisha yenyewe.

Sikujua kama ndiye alihusika. Mtu huyo alihamia Tabora kisha mwaka 2016.
 
Back
Top Bottom