Ndiyo maana niliwahi ng'atwa na nyuki nikaona si jambo la kawaida.
Iko hivi, mwaka 2021 mwezi wa tano, nikiwa natoka Kashishi (wilaya ya Kaliua) kwenda shule ya Sekondari Ilege (kupitia Kijiji cha Sasu), nilipokaribia kijiji cha Sasu, kulikuwa na kijipori flani hivi, ghafla niling'atwa mdomoni na nyuki maana kichwani nilikuwa na helmet.
Niliwashwa mwili mzima baada ya kung'atwa na nyuki. Kwa wenyeji wa kijiji hicho, ukiikamata njia ya kutoka Sasu kwenda shuleni Ilege, nilikimbiza pikipiki kwa kujikaza huku nawashwa lakini uvumilivu ulinishinda. Nilishuka kwenye pikipiki na kuanza kujikuna mwili mzima, hadi nilivua shati (hapo nipo njiani ila hakuna watu wengi).
Punde alitokea mzee akaniuliza nini kinanisibu, nilipomjibu kuwa nimeng'atwa na nyuki alicheka sana na kusema "nyuki wa Tabora wanakukaribisha mkoani kwao" kisha akasepa.
Nilijikuna baadae nikaona ujinga, nilitembeza pikipiki huku nawashwa ngozi yote ila nikasema sijikuni. Mpaka nafika shuleni, ngozi ilikuwa inawasha.
Kabla ya Kung'atw na nyuki huyo, nilizoea uking'atwa na nyuki utaumia eneo alilokung'ata pekee na baada ya hapo patavimba, lakini huyo akawa na utofauti huo.