Kwanini Ethiopia haijawa Super Power ya Afrika?

Kwanini Ethiopia haijawa Super Power ya Afrika?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mwalimu wa Historia alitumbua kuwa chanzo kimojawapo cha udumavu wa bara la Afrika kimaendeleo ni ukoloni wa Kimagharibi!

Lakini pia alitufundisha kuwa Ethiopia haikutawaliwa na Wazungu. Labda ndiyo maana Waafrika walipachagua pawe makao makuu ya AU?

Lakini nilisahau kumwuliza kuwa ikiwa Ethiopia haikutawaliwa na wageni, kwa nini siyo super power alau barani Afrika?

Kuna anayeweza kunisaidia jibu?
 
Kuendelea au kutoendelea kwa mwafrika hakuhusiani na mzungu. Ni viongozi wa afrika tu wanatumiaka hicho kichaka kukwepa uwajibikaji.

Kutoendelea kwa Afrika sababu kuu ni Rushwa na kukosa akili kwa viongozi na wananchi wa Afrika full stop
 
Mwalimu wako wa historia amepotoka, akakupotosha na wewe.

Kutawaliwa au kutotawaliwa inaweza kuwa incentive au disincentive to economic growth, na sio the only significant factor to being a superpower.
 
Kuendelea au kutoendelea kwa mwafrika hakuhusiani na mzungu. Ni viongozi wa afrika tu wanatumiaka hicho kichaka kukwepa uwajibikaji.

Kutoendelea kwa Afrika sababu kuu ni Rushwa na kukosa akili kwa viongozi na wananchi wa Afrika full stop
Umemaliza mkuu
 
Haijawahi kuwa na viongozi kuifanya super power, jiografia mbovu,
 
Tanzania ndio superpower 🤣🤣 maajabu haya
 
Ewaaa,,,, nyingine land alienation,,,,

Ongeza ongeza zifike kumi
Kumi? Mbona ushazitaja nyingi?

Acha niongezes na hii:
CATTLE CONFISCATION!

Au unataka na maelezo? Nafikiri ilikuwa ni topic ya form 2, if I have not mistaken!
 
Iweke vizuri mkuu sema poor geagraphical condition 😀😀😀
Nilikuwa mpenzi wa somo la Historia lakini Mwalimu hakutufundisha hii point!😄Wewe umeitoa wapi? Hebu elezea kidogo, usije ukawa unatulisha point ambazo hazipo kwenye syllabus!
 
Kumi? Mbona ushazitaja nyingi?

Acha niongezes na hii:
CATTLE CONFISCATION!

Au unataka na maelezo? Nafikiri ilikuwa ni topic ya form 2, if I have not mistaken!
😀😀😀😀😀 Essay iliyoshiba ni point nane mbili za nyongeza eti cattle consfication hii kitu inanikumbusha mbali sana
 
Nilikuwa mpenzi wa somo la Historia lakini Mwalimu hakutufundisha hii point!😄Wewe umeitoa wapi? Hebu elezea kidogo, usije ukawa unatulisha point ambazo hazipo kwenye syllabus!
😀😀😀😀 Hiyo ipo mkuu Ethiopia ni semi arid haipati mvua za kutosha kwahiyo mazao hayastawi na ukame hivyo haiwezi kuwa super power au wataka nijazie na mifano?
 
😀😀😀😀 Hiyo ipo mkuu Ethiopia ni semi arid haipati mvua za kutosha kwahiyo mazao hayastawi na ukame hivyo haiwezi kuwa super power au wataka nijazie na mifano?
Ok! Sawa mkuu! Sijui tuingie kwenye ubishi?

Mbona Israel ni jangwa lakini ni moja ya nchi zinazojiweza? Sijui kama nayo ni super power!

Mbona Misri ina kaukame lakini ipo vizuri kuizidi Ethiopia japo nayo siyo super power?

Mkuu, mbona nchi za Kiarabu ni jangwa lakini ni tajiri? Ethiopia Haina mafuta kama nchi za Kiarabu, lakini naamini ina rasilimali mbadala ambazo zingeweza kuifanya super power!
 
Mwalimu wa Historia alitumbua kuwa chanzo kimojawapo cha udumavu wa bara la Afrika kimaendeleo ni ukoloni wa Kimagharibi!

Lakini pia alitufundisha kuwa Ethiopia haikutawaliwa na Wazungu. Labda ndiyo maana Waafrika walipachagua pawe makao makuu ya AU?

Lakini nilisahau kumwuliza kuwa ikiwa Ethiopia haikutawaliwa na wageni, kwa nini siyo super power alau barani Afrika?

Kuna anayeweza kunisaidia jibu?
neno ukolon lina maana nyingi si tu mzungu kumcorony mwafrica ht wa africa sie kwa sie tuna coroniana mfano super power family 1 inaingia madarakan inapga wanajinufaisha wao tu watu wengine wanaptia hal ngum ya uchum mfano kenya familia ya uhuru inamilik ardh karbia robo nzima ya nchi hat nchi za ulay ukienda ma3ndeleo ni ya vitu sana ila raia wapo chal na wengine wananufaik zaid wa kweny systeqm mfano familia za kifalme au powerful family mwaka juz waingerez weng walipg kula mfumo wa kifalme uondoshwe hawautak vitu km ivo pia hat hap africa au ethiopia unaona ajanyonya mkolon ila kuna wajanja wamenyonya wenzao kias unakut mapigano hayaish na hal dun vle vile hat waliotawaliw weng wamerejshew madarak miak ming lakn hal unakut bado iko vle vle au imezid pale adui mkubw wa maendeleo ni rushwa kushinda hat mkolon kwakua ukosesha usaw na kulet upendeleo ndioman china waliweka shelia kal rushwa wiz wa mal ya umabni kunyongwa ndioman uchum wake umepaa ghafla nae alitawaliw na mjapan kumbuka ila saiv ana uwezo kumpita mjapan aliomtawala
 
Back
Top Bottom