Kwanini Freeman Mbowe hafungwi pingu kama washtakiwa wenzake? Yeye si ndio kinara, sponsor, na mastermind wa tuhuma zao?

Kwasababu siyo gaidi
 
Kimantiki wala hatupingani wala hatutofautiani...

Labda tunatofautiana katika namna na lugha ya kulielezea tu...
 
Kama alianguka kwenye ngazi akiwa mwenyewe, undhani hapo ataweza kuwachomoka vipande hivyo...
 
hapa ndipo utaona maajabu ya nchi yetu, UGAIDI wa sh laki sita - ifike hapala tuwe serious watanzania, hii ni aibu kwa nchi yetu tunajipaka matope wenyewe.
 
Kumbe akija mtu kwangu akala chakula na kunywa maji akaondoka halafu badae akakamatwa kwa tuhuma za ugaidi na mimi ntahusishwa kuwa ni Gaidi??
 
Ama watuhumiwa wote wafungwe pingu au watuhumiwa wote wasifungwe pingu.

pasiwepo na ubaguzi miongoni mwa watuhumiwa.

..mimi ni shabiki wa Chadema lakini jambo hili linanichukiza.
Mara unajiita mwanachama wa CHADEMA mara mshabiki tena,

In short CHADEMA hatuna kilaza wa aina yako.
 
Akifungwa hizo pingu wewe inakuongezea nini labda! na asipofungwa hizo pingu wewe unapungukiwa wapi kumbe??
 
Kwani mpaka ujitambulishe kwa itikadi yako ya Chama? kwani hapa JF ni mahali pa kujitambulisha itikadi zetu za chama? Wewe toa hoja basi, hayo mengine ya Chama baki nayo moyoni mwako.

..sio jinai kuwa shabiki wa chama fulani.

..kwa hiyo, una uhuru wa kujitambulisha kuwa unashabikia chama fulani.

..pia unayo haki ya kutojitambulisha kuwa unaunga mkono chama cha siasa.

..kitu kibaya ni kubaguana au kudhulumiana kutokana na itikadi za vyama.
 
Hata wakina adamoo hawajathibitika kuwa ni magaidi.

Sasa kwanini wao watiwe pingu, huku anayetuhumiwa kuwatuma na kuwafadhili hatiwi pingu?
Wale ni makomandoo .....mafunzo yao hali juu lazima kuwadhibiti....buku 7 buana
 
Mbowe sio gaidi aachiwe!
 
Kesi ya kubumba hiyo
 
Madhumuni ya PINGU ni kumfanya mhalifu ama asitoroke au asilete madhara kwa askari. Je katika hayo mawili, Mbowe anaweza akafanya lipi?
 
Shida ni pale unapowasilisha hoja ya Chama kama excuse fulani vile. Mfano unasema, japo mimi ni Chadema lakini hapa chadema imekosea. kwanini usiseme tu hapa Chadema au CCM imekosea bila kutanguliza hiyo excuse
 
Madhumuni ya PINGU ni kumfanya mhalifu ama asitoroke au asilete madhara kwa askari. Je katika hayo mawili, Mbowe anaweza akafanya lipi?

..kulingana na maelezo ya polisi na serikali Mbowe anaweza kutoroka na anaweza kuwadhuru askari.

Why? Kwanini?

1. Viongozi wa serikali wamedai kwamba Mbowe aliwahi kutoroka nchini kabla hajakamatwa.

2. Serikali na Polisi wanadai kwamba Mbowe na wenzake walikuwa wanapanga kuwadhuru viongozi wa serikali, kulipua vituo vya mafuta, etc etc.

..Maana ya madai ya polisi, na serikali, ni kwamba Mbowe na watuhumiwa wenzake ni watu hatari.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuuliza hayo maswali kwani majibu yapo waziwazi unayapata tu kwa kuangalia picha. Mnafikili hao askali magereza ni vilaza kama nyie??
Sawa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…