Kwanini gari yako ikiwa imepigwa rangi mara ya pili inakuwa ngumu kuuzika?

Ndugu, kwanini gari ikirudiwa rangi inasumbua sana kuuzika? Gari haina ajali yeyote, haigongi chini, haina weird noises kwenye engine, interior iko safi kabisa, lakini haitoki sababu tu nimeirudia rangi?
Mara nyingi watu wanapiga rangi cheap. Unakuta mtu anataka kuuza gari ila ina scratches all over, basi anapiga rangi cheap then anaiweka sokoni. Ukinunua hii baada ya miezi kadhaa rangi inababuka.
Hata mimi sinunui gari iliorudiwa rangi afadhali ninunue nikapige rangi mwenyewe.
BTW si watu wengi wana uwezo wa kujua gari iliorudiwa rangi.
 
Weka picha tuone hiyo rangi ilipigwaje kwanza. Isije ikawa ulipeleka kwa fundi maiko akajaza maputi
 
Ndugu, kwanini gari ikirudiwa rangi inasumbua sana kuuzika? Gari haina ajali yeyote, haigongi chini, haina weird noises kwenye engine, interior iko safi kabisa, lakini haitoki sababu tu nimeirudia rangi?

Kwanini uipige rangi ??, Unaficha nini kwa kuipiga rangi??, mbona vitu vingine hujavikarabati isipokuwa rangi tu??-- hayo ni miongini mwa maswali mteja anaweza kujiuliza.
 
Watu huwa na hofu na vitu viwili vitatu...

1. Gari imepigwa rangi upya kwa kuwa ilipata ajali iwe kubwa au ndogo.

2. Ubora hafifu wa rangi iliyotumika

3. Mengineyo kama gari kuwa ya uizi, kukwepa process za kubadili kadi ya TRA endapo gari imebadilishwa aina ya rangi iliyokuwepi wakati ikiingizwa nchini
 
Mara nyingi watu wanapiga rangi cheap. Unakuta mtu anataka kuuza gari ila ina scratches all over, basi anapiga rangi cheap then anaiweka sokoni. Ukinunua hii baada ya miezi kadhaa rangi inababuka.
Hata mimi sinunui gari iliorudiwa rangi afadhali ninunue nikapige rangi mwenyewe.
BTW si watu wengi wana uwezo wa kujua gari iliorudiwa rangi.

Hapo kwenye cheap!
Mimi nimeuza gari langu ambalo nilipiga rangi mkono mmoja wanaita ile kwenye professional garage na rangi original. Huwezi kulitambua hata, ila tu ikumbukwe lengo la rangi ilikua tu kuongeza shining ila sio ajali.

Hata ya magari tunaagiza nje baadhi kupigwa mkono mmoja au polish ili kuleta uhalisia, sema hapa home kuna mabingwa wanachukua gari la ajali alafu rangi yenyewe inapigwa kihuni.

Huko show room kuna magari mengi tu ya rangi mkono mmoja mbona na tunayanunua [emoji16]
 
Kwanini uipige rangi ??, Unaficha nini kwa kuipiga rangi??, mbona vitu vingine hujavikarabati isipokuwa rangi tu??-- hayo ni miongini mwa maswali mteja anaweza kujiuliza.
Personally, sipendi gari iwe imepauka. Inakuwa na muonekano mbaya
 
Back
Top Bottom