Kwanini gasi asilia haitumiki kwenye magari nchini?

Kwanini gasi asilia haitumiki kwenye magari nchini?

Duksi

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
229
Reaction score
576
Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwan na rasilimali ya gesi asilia.

Tanzania inakadiriwa kiwa na gesi ya trilion 57 futi za ujazo (57 tcf) huko Mtwara na Lindi.

Mwaka 2012 serikali iliingia mkataba wa kujenga bomba la gesi kutoka mnazibay Mtwara mpaka Dar lenye urefu kilometa 542 kwa gharama ya shilingi trilioni 3 ambazo zilikuwa mkopo kutoka Exim China.


Bomba lilikamilika oktoba 2015.

Gesi hii inatumika kuzalisha umeme kupitia vituo vya songas ubungo, kinyerezi na vingenevyo ambayo imesaidia uwepo wa umeme wa uhakika kuacha ule wa kutegemea maji.

Nafikiri kuna fursa kubwa sana ya kutumia gesi kwenye magari ambayo kwa sasa inatumika kwa uchache sana.

Nadhani ni wakati wa serikali kuwekeza kwenye miundombinu na kuweka sera zitakazochochea matumizi ya gesi asilia inayopatikana hapa nchini kwenye magari. Kuna magari yanayotengenezwa kutumia gesi asilia. Nchi za China, Iran, India, Argentina, Brazil na Italia zinaongoza kitumia magari haya kwa miaka ya 2016. Pengine changamoto ya usafirishaji wa gesi hii kwa magari kwasababu ni nyepesi ndio inafanya isitumike sana lakini inawezekana.

Mtazamo ni;
1. Vituo vya usambazaji gesi asilia (gas station) viwe vingi haswa dar
2. Kuwepo na punguzo la kodi kwa magari yanayonunuliwa (imported) ambayo yanatumia gesi asilia ili kuvutia wengi kutumia gesi hii.
3. Karakana za kubadili magari ya petrol kutumia gesi asilia ziongozwe na bei ziwe rafiki.

Nadhani kwa kutumia gesi asilia itasaidia kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumwa uarabuni kununua petroli ambayo bei yake inazidi kupaa kwenye soko la dunia. Hii itasaidia hata kupandisha thamani ya shilingi yetu.

Vile vile itapunguza makali ya maisha kwa wananchi wengi kwakuwa gesi asilia ni gharama nafuu kuliko petroli.

tanzania-gas.gif


images.jpeg


images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom