Kwanini Hairuhusiwi kupiga picha za TV mahakamani?

Kwanini Hairuhusiwi kupiga picha za TV mahakamani?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Jamani naomba kufafanuliwa sababu hasa inayosababisha wapiga picha za
Runinga na wengineo wasiruhusiwe kupiga picha wakati hakimu/Jaji anaendesha
kesi, kutoa hukumu n.k

Kama mahakimu wetu ni waadilifu kwanini iwe tatizo? Kama mataifa mengine yanafuata
utaratibu huu tunaoutumia binafsi naona sio busara kuwafuatisha, tena iruhusiwe tu hata
kwenye katiba mpya kuwa iwapo kuna chombo kinaweza kurusha 'Live' kesi yoyote basi
kifanye hivyo.

Kuna ubaya gani tukishuhudia kesi zinavyoendeshwa mahakama kuu kama tunavyoshuhudia
Bunge linavyoendeshwa DODOMA? Pale sio polisi kwamba kuna upelelezi unaendelea.
Ingekuwa vizuri sana kama kuna TV au REDIO ambayo ingekuwa na kipindi KUTOKA MAHAKAMANI,
KUTOKA MAHAKAMA KUU, HUKUMU...... n.k.

Binafsi naona huo ndio uadilifu.
 
mkuu
ni sheria zilizopo,kwa kuwa tupo katika marekebisho y akatiba na hili tunaweza kulitazama kwa kuwa sheria zetu zinatungwa kwa kutazama sheria mama(katiba).

ikirekebishwa hii,utaona live bila chenga
 
Kuhusu Mwenendo wa kesi kurekodiwa kieletroniki ni jambo muhimu sana ili kuepukana
na tabia ya RUSHWA ya baadhi ya mahakimu na Majaji kwani kumbukumbu zilizohifadhiwa kielektroniki
(Picha na Sauti) itasaidia sana kwenye Rufaa na marejeo ya kimahakama ili kutenda haki, itaepusha
upotoshaji wa kumbukumbu unaofanywa na mahakimu/majaji kwa maslahi yao binafsi au shinikizo
toka kwa watawala. Lakini kumbukumbu hizo lazima zipate ithibati ya kimahakama na zitunzwe na mahakama
na ziwe zinapatikana kwa urahisi kwa wananchi. Hata hivyo siyo sahihi kwa mwenendo wa kesi yeyote kurushwa
live kama mechi ya mpira au Bunge, Sheria na utendaji wa haki ni tasnia ya kitaalamu ambayo ili kutenda haki
hakimu hatakiwi kuingiliwa kwa vyovyote katika kutoa uamuzi wake, kuweka hadharani mwenendo wa kesi kabla ya
kesi kumalizika huweza kuathiri uamuzi wa hakimu kwani wakati mwingine maoni ya mtangazaji na wananchi wa
kawaida ambao sio wataalamu wa sheria huweza kumshinikiza hakimu kutoa hukumu ya kuridhisha maoni yao badala
ya kutenda haki. Mfano ni kesi moja ya aina yake ambayo ni maarufu Duniani kote, kesi ya YESU KRISTO, Jaji Pilato
hakumpata mtuhumiwa na hatia(ACQUITTAL), lakini kutokana na shinikizo la watawala na baadhi ya wananchi alimuadhibu(SENTENCED). Huu ndio umuhimu wa kuiachia mahakama iwe huru.
 
Back
Top Bottom