Kwanini Haji Manara akihojiwa anatokwa povu sana?

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
5,286
Reaction score
5,421
Naomba kujuzwa nisijepata dhambi kwa kumfikiria mtu vibaya ni bora kuuliza,huyu bwana ni msemaji wa timu ya simba nimekua nikifuatilia sana mahojiano yake na vyombo vya habari katika vipindi vya michezo,si kwenye tv wala redio huyu jamaa akihojiwa anatokwa povu la haja,yaani hata mtangazaji ajishushe vipi na hata akiulizwa maswali malaini kabisa bado atatokwa povu,kuna kipindi alikua anahojiwa na maulidi kitenge jamani ilikuwa balaa,jamaa anarusha mate kama koboko,jana kupitia Tv 1 alikua anahojiwa kistaarabu tu kuhusu tetesi za kina emmanuel okwi akaanza kutema povu,nimepata wasiwasi sana hata na elimu yake,jana kuna kitu alikua anakikosoa na kukitetea at the same time ilikua ishu ya tetesi za usajili ambazo hata ulaya zipo,nijuzeni ndugu zangu tatizo la haji ni nini?kwanini hutoa povu sana akihojiwa?kwa sasa hata vyombo vingine vimebadili utaratibu na kuamua kumhoji mussa mgosi,je ni hasira?hulka?au kichaa?
 
kwa mujibu wa maelezo yako wewe ndio unamwaga povu

oooh mara kitenge mara Tv1 mara kichaa

PUNGUZA JAZBA ACHA KUMWAGA POVU
 
Hapo hujaelewa nini?kitenge yuko efm redio na tv 1 ni kituo cha television
 
hata mimi huwa najiuliza hayo maswali mana hata nikisikiliza akihojiwa magic fm ni the same answers
Watu tunaofuatilia michezo ni rahisi kugundua hili jambo,sijui ana tatizo gani haji.
 
Ukiwa na akili ya kitumwa kazi yako kufuatilia mwanaume kasema nini. Unampigia baniani magoti unawezaje kuwasema wengine.?
 
Duh we jamaa taahira kweli,sasa niache kufuatilia michezo?kama hutaki msikike kwenye redio or tv msipokee simu na muache hizo kazi haraka,unanipangia namna ya kuishi?sijui kwanini watu dizain yako mnaishi wanaondoka watu wa maana
 
Tofauti ni kwamba kuna mmoja anaomba kuinunua timu na mwingine anapigiwa magoti na vichaa.
 
Huyu mwingine hamia kwa Haji kwani upo obssesed naye. Si mna viongozi wenu?Kichaa mpiga magoti.
 
Naomba kujuzwa nisijepata dhambi kwa kumfikiria mtu vibaya ni bora kuuliza,huyu bwana ni msemaji wa timu ya simba nimekua nikifuatilia sana mahojiano yake na vyombo vya habari katika vipindi vya michezo,si kwenye tv wala redio huyu jamaa akihojiwa anatokwa povu la haja,yaani hata mtangazaji ajishushe vipi na hata akiulizwa maswali malaini kabisa bado atatokwa povu,kuna kipindi alikua anahojiwa na maulidi kitenge jamani ilikuwa balaa,jamaa anarusha mate kama koboko,jana kupitia Tv 1 alikua anahojiwa kistaarabu tu kuhusu tetesi za kina emmanuel okwi akaanza kutema povu,nimepata wasiwasi sana hata na elimu yake,jana kuna kitu alikua anakikosoa na kukitetea at the same time ilikua ishu ya tetesi za usajili ambazo hata ulaya zipo,nijuzeni ndugu zangu tatizo la haji ni nini?kwanini hutoa povu sana akihojiwa?kwa sasa hata vyombo vingine vimebadili utaratibu na kuamua kumhoji mussa mgosi,je ni hasira?hulka?au kichaa?

Naomba nikujibu ' Kitaaluma ' zaidi Mkuu. Ni kweli kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara huwa na tabia ya ' kupovuka ' sana pale anapofanyiwa ' interview ' na Media. Kwanza naomba nikuhakikishie tu kuwa siyo kweli kuwa hufanya hivyo kwa Vyombo vyote vya Habari vinavyomuhoji bali ni baadhi yake.

Udhaifu wa Manara.

Kwanza tambueni kuwa Manara ni Mwanahabari tena mzuri tu na mweledi ila hata Mimi nasikitika na hata kumshangaa pia kwa jinsi anavyokuwa ' anapovuka ' kwa Wana ' tasnia ' wenzie. Tatizo kubwa linalomsumbua Haji Manara nadhani ni la ' Kisaikolojia ' zaidi kwani huwa hapendi Klabu yake ya Simba iwe inasemwa vibaya na Wadau iwe ni kwa mustakabali wa Timu kama Timu kufanya vizuri na ukweli wa Kiutawala wa Klabu na yeye anachokitaka tu ni kusikia Simba inatamkwa tu kwa mema huku ikisifiwa kitu ambacho lazima leo nimshauri Msemaji wangu wa Klabu yangu pendwa ya Simba Haji Manara kuwa lazima ajue kuwa kama Simba ikisifiwa basi pia ajue kuna siku Simba itasemwa vibaya hivyo akubaliane positively na hali zote hizo na zitamjenga na kumkomaza zaidi kuliko sasa anavyoonekana kuwa na yeye ni wa ' hovyo hovyo ' na kututia mashaka tunaomjua kama ni kweli ametokea katika Familia ya Soka. Haji Manara ajifunze kuwa Msemaji na siyo Mropokaji.

Udhaifu wa Wanahabari wanaomhoji.

Kama Waandishi wa Habari na wao hawatajirekebisha juu ya hili basi nina uhakika 100% kila siku watakuwa wanapata wakati mgumu sana wafanyapo ' interview ' na Haji Manara. Kwanza hao Waandishi wengi wanaomhoji Haji Manara huwa wanasahau kitu muhimu sana katika tasnia ya Uandishi wa Habari na Utangazaji kiitwacho ' objectivity ' nikimaanisha kuwa wanatakiwa kuwa ' katikati ' na wasionyeshe upande wowote wa ' mahaba ' yao katika Timu mbili hizi kubwa ( Dar es Salaam Titans ) Simba na Yanga lakini ni ukweli usiopingika kuwa Waandishi wengi wanaomhoji Haji Manara kwanza huanza kwa ' kumkejeli ' hasa kwa aina ya maswali yao ' chokozi ' na ya ' kinafiki ' Kwake kitu na bahati nzuri hata yeye Haji Manara anawajua kwani hata hao Waandishi wa Habari kwa ' upopoma ' wao uliotukuka huwa wanajitangaza waziwazi kuwa wanashabikia Klabu fulani kubwa kitu ambacho ' psychologically ' humfanya Haji Manara kuwa ' emotional ' juu yao na hatimaye yeye ' kupovuka '.

Nini kifanyike?

Namwomba Haji Manara na hawa Waandishi wa Habari hizi za Michezo hapa Tanzania warudi kupitia ' maadili ' yao ya Kiutendaji na Kiueledi kisha wabadilike haraka kwani kiukweli wote wanachokifanya hakina ' afya ' katika ' tasnia ' na sana sana tu kinashusha ' Credibility ' zao na za Taasisi wanazozifanyia. Haji Manara jua kwamba Wewe ni kama ' Jalala ' ambalo kila aina ya ' uchafu ' utatupwa Kwako hivyo kuwa mvumilivu na kubaliana na yote kwani ndiyo Kazi yako hiyo hivyo acha kupandwa na ' Jazba ' kwani utajiaibisha lakini pia na nyie Waandishi wa Habari za Michezo ' badilikeni ' na acheni ' uswahili ' wenu bali fuateni ' kanuni ' za Kazi zenu kwani haya ' mahaba ' yenu ya waziwazi Kazini yatawaharibia na mtazidi ' kudharaulika '.

Kila la kheri Mkuu.
 
Sina neno la zaidi,asante mkuu umedadavua kiume sana,kuna vikojozi wameshindwa kuona mantiki ya huu uzi.
 
Vikojozi huwa wanakukojolea ama sivyo usingewajua. Kukojolewa inaelekea ni taaluma yako tokea Tanga.
 
Back
Top Bottom