Nas Mapesa
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 5,286
- 5,421
Naomba kujuzwa nisijepata dhambi kwa kumfikiria mtu vibaya ni bora kuuliza,huyu bwana ni msemaji wa timu ya simba nimekua nikifuatilia sana mahojiano yake na vyombo vya habari katika vipindi vya michezo,si kwenye tv wala redio huyu jamaa akihojiwa anatokwa povu la haja,yaani hata mtangazaji ajishushe vipi na hata akiulizwa maswali malaini kabisa bado atatokwa povu,kuna kipindi alikua anahojiwa na maulidi kitenge jamani ilikuwa balaa,jamaa anarusha mate kama koboko,jana kupitia Tv 1 alikua anahojiwa kistaarabu tu kuhusu tetesi za kina emmanuel okwi akaanza kutema povu,nimepata wasiwasi sana hata na elimu yake,jana kuna kitu alikua anakikosoa na kukitetea at the same time ilikua ishu ya tetesi za usajili ambazo hata ulaya zipo,nijuzeni ndugu zangu tatizo la haji ni nini?kwanini hutoa povu sana akihojiwa?kwa sasa hata vyombo vingine vimebadili utaratibu na kuamua kumhoji mussa mgosi,je ni hasira?hulka?au kichaa?