Kwanini Hamza aliwalenga Polisi tu?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Hilo ndio swali kuu kwa sasa. Kwanini Hamza alikuwa akiwapiga risasi polisi tu na sio raia wengine?

Mashuhuda wanasema Hamza alikuwa akisema anawataka Polisi awamalize na hakuwa na dhamira mbaya na raia wengine waliokuwepo mazingira yake. Kama kuna raia yoyote alipigwa na risasi huenda ilikuwa ni bahati mbaya au alishukiwa kuwa sehemu ya polisi.

Je, Hamza alikuwa na msongo wa mawazo baada ya kufilisika? Sasa kwanini awatandike risasi polisi tu?

Je, Hamza alikuwa gaidi? Sasa kwanini awatandike risasi polisi tu?

Hamza pamoja na kuwa alikuwa kada na mfadhili wa CCM kwa miaka kadhaa mpaka mauti yalipomkuta, bado alionesha hasira na chuki dhidi ya jeshi polisi wakati wa hili tukio.

Kwanini Hamza alikuwa akiwalenga polisi tu?
 
Angekua na lengo la kuua kika raia aliye onekana mbele yake, basi leo hii dunia yoye ingemuongelea yeye tu! Maana wale abiria wa kwenye daladala wangepona wachache sana.
 
Hili swali litajibiwa vizuri na Tume Huru ya kiuchunguzi itakayoundwa kufuatilia sababu ya lile tukio.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hamza ni muendelezo wa gaidi la kibiti na uamsho
 
Reactions: G4N
Hamza pamoja na kuwa alikuwa kada na mfadhili wa CCM kwa miaka kadhaa mpaka mauti yalipomkuta, bado alionesha hasira na chuki dhidi ya jeshi polisi wakati wa hili tukio.
Mkuu hapa umeongea kiutu uzima sana. Polisi na CCM hawatengamani. Hata mimi nimeshangaa kuwaua wanaCCM wenzake. Tusubiri ripoti ya uchunguzi wa polisi; lakini kuna tetesi kuwa polisi walimpora madini yake (kama kawaida yao) ndipo akapata hasira ya kumlipua kila polisi atakayekutana naye. Polsii wa nchi hii ni majitu wa ajabu sana.
 
Mimi ninachowaomba Wazazi msituzalie watoto wa aina hii ya Simon sero. Wasiojua hata kutofautisha picha zilizopigwa na YASHICA na zile zinazotokana na CCTV cameras.
 

Ndiyo tabia ya magaidi.
Gaidi hubeba mabomu kutoka buguruni anapita kariakoo anaenda kujilipua ubalozini. Gaidi halipui hovyo hovyo anafanya kulingana na mission na alivyoelekezwa na wakuu wake ktk imani yake ya kigaidi. Gaidi halipui hovyo hovyo tu ili aue na watu wake?

Wanaojilipua kokote huwa mara zote wanalenga watu fulani hasa police wanajeshi balozi. Hawezi jilipua hovyohovyo ili apoteze uhalali wa kutetewa?
 
Mbona video zinasema kila kitu kuhusu Hamza! Au kuna jingine?
 
Mkuu hiyo ripoti yenyewe itakuwa haina ukweli wowote watajipendelea wenyewe, Kesi ya ngedere unaipeleka kwa nyani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…