Kwanini hapa Tanzania kama haujui kiingereza watu wanasema haujasoma hata kama umesoma?

Kwanini hapa Tanzania kama haujui kiingereza watu wanasema haujasoma hata kama umesoma?

Kumbuka ambao hawajui kiingereza na wanatamba na lugha zao ni mataifa tajiri. Bidha wanazozalisha wanaandika kwa lugha yao na unabidi ujifunze hiyo ludha ili uelewe kilichoandikwa. Wewe na kiswahili chako unazalisha nini ili uwauzie wajifunze lugha yako? Kiingereza ni muhimu ndio maana ukikijua unaonekana ni msomi kumbe ni mbwembwe tu! Angalia English na French zote ni za mataifa makubwa yanayojulikana duniani, ukitaka ujulikane na usiwe na shida duniani zijue hizo lugha.
Mara nyingi wasiojua Kingereza tunajifichia kwenye hii sababu ya kitoto
 
Kumrekebisha mtu ambae anafanya makosa huku yeye akiamini 100% kuwa yupo sawa sio kazi rahisi.

Cha msingi umemwelewesha. Kama akikubali kujifunza sawa, akikataa mwache abaki na ujinga wake.
Walimu tunapitia magumu sana😂, ila ndio hivo “You can lead a horse to water, but you can't make him drink”.
 
Halafu sasa chakushangaza kiingereza huwezi ukakijulia shuleni

Labda kama unasoma international school
 
Angalua tu nchi tatu za Africa mashariki, Tz tupo nyuma kitaaluma kwa kuwa tuliweka sana kiswahili mbele. Mtu anafeli sekondari sio kwamba hajui ila lugha. Interview unapigwa chini na wenzetu wanachukuluwa, sio wanapendelewa ila kwao lugha inapanda. Tumshukuru Mkapa alijitahidi sana hasa katika shule za medium. Sasa ndio tunaona umuhimu wa kiingereza ila "too late".
 
Yaani hii nchi MTU anayejua kiingereza ndo MTU anayekubalika Kama msomi.

Inafikirisha Sana hili jambo. Tunapima level ya intelligent kwa kuangalia lugha.

NB: Vijana jifunzeni kiingereza ili msipitwe na maarifa maana maarifa mengi yapo katika lugha ya kiingereza.
Sasa bro, elimu yq juu inatolewa kwa kizungu, sasa ulielewaje masomo yako makuu, na, wakati lugha iliyotumika huiwezi!.? Ndio maana, tunasema kwa bongo, kama kizungu hakiendi, basi wewe kilaza!it'd just simple as that, hii formula ni kwa bongo tu!
Ila kwa jirani zetu Kenya, lugha inafundishws vzr tu, watu wanabonga kizungu na vichwani zero tu, ni kama mzsramo kuzungumza ki Swahili na ameishia LA pili!
 
Utumwa wa fikra , wachina wanaopewa tenda zooote huko nchini hawajui kiingereza wala kiswahili lakini kila kitu wao tu, kingereza ni kama kihaya na kinyakyusa tu period.
 
Kutumia fake ID kunawaokoa watu wengi sana kupitia janga la aibu.

Tupo kwenye taifa ambalo mtu anaye jua English ndiye anahesabika kuwa na akili na maarifa ya kutosha wakisahau kwamba English ni Lugha tu ambayo mtu anaweza kuzamia hata Zambia akarudi bongo anaijua vyema.

Ni aibu kubwa sana kama watu wenye mawazo ya namna hii ndio tunawategemea kuja kuwa viongozi kulifikisha taifa mbali.

Nimesikitika sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Yaani hii nchi MTU anayejua kiingereza ndo MTU anayekubalika Kama msomi.

Inafikirisha Sana hili jambo. Tunapima level ya intelligent kwa kuangalia lugha.

NB: Vijana jifunzeni kiingereza ili msipitwe na maarifa maana maarifa mengi yapo katika lugha ya kiingereza.
Naona unachanganya mada. Kuwa ' intelligent' kwako ndio kuwa msomi?
 
Back
Top Bottom