Kwanini hata huko mikoani bei za bidhaa hususan vyakula zinapangwa kutoka soko la Dar?

Kwanini hata huko mikoani bei za bidhaa hususan vyakula zinapangwa kutoka soko la Dar?

ezekeo

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
63
Reaction score
158
Nimeishi mikoa kadhaa tofauti na dsm kwa muda mrefu huku nikihama kutoka mkoa mmoja hadi mwingine...

Ila kitu nilichokigundua ni kwamba bei za bidhaa hususan zile zisizosafirishwa kutoka mbali bei zake zinapangwa kwa kulinganishwa na bei za soko la dsm

Bidhaa Kama unga,mchele,nyama,maharagwe,mafuta ya alizeti,n.k bei zake huwaga zinafanana na bei za dsm ama tofauti huwa ni kidogo sana endapo utaomba punguzo.

Huwa najiuliza kwamba inawezekanaje bei ya nyama ya geita,mwanza, Mara, simiyu na shinyanga iwe sawasawa na bei ya nyama ya dar es salaam ikiwa ng'ombe zinazochinjwa dsm huko mikoani ndiko zinakotokea? Ni Nani huwa akipanga hizi bei?

Inawekanaje bei ya nyama ya ng'ombe anaeswagwa kutoka kwa mfugaji kwenda machinjioni iwe sawa sawa na bei ya nyama ya dsm ambako ng'ombe anasafirishwa kwa marori kwa siku kibao huku ng'ombe akilishwa njiani,mdadani pugu hadi atakapopata mteja ambae nae atamsafirisha kwenda vingunguti au pale ukonga mazizini ambako pia kutakuwa na gharama nyingine hadi kuchinjwa na nyama kusafirishwa tena kwenda mabuchani.

Kuna wafanyabiashara kadhaa nilijaribu kuwauliza kwamba inakuwaje bei zao zina ufanano na bei za dsm wakanijibu kuwa utaratibu wao ndio upo hivyo yaani kila mfanyabiashara wa aina fulani ya bidhaa ni lazima awe anajua bei ya kuuzia dsm ipoje ili na yeye apange bei yake zifanane bila kuangalia kama atapata faida kubwa kupindukia.


Hivi huwa kuna mamlaka za kiserikali za kudhibiti na kupanga bei za bidhaa au suala la bei huwa linapangwa na mfanyabiashara mwenyewe? Na Kama ipo hiyo mamlaka ya udhibiti huwa inayaona haya?
 
Mfano cement ya darngot unanunua MTWARA Tshs15000/- then dar unakuta 14500

Cjui ndio demand and supply
 
Back
Top Bottom