Kwanini hatuhisi kama Dunia inazunguka kasi ya maelfu ya kilomita kwa saa?

Kwanini hatuhisi kama Dunia inazunguka kasi ya maelfu ya kilomita kwa saa?

Red black

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
18,719
Reaction score
60,636
Kwanini hatuhisi kama Dunia inazunguka kasi ya maelfu ya kilomita kwa saa?

1787492054437.png
 
Ni kwasababu sisi pamoja na kila kitu kilichopo duniani (hewa, majengo, bahari, wanawake nk) tunazunguka kwa kasi ile ile moja kwa moja. Hatuhisi mwendo isipokuwa tu pale kunapokuwa na mabadiliko ya kasi (acceleration) au kusimama ghafla.
Ni sawa na kwenye basi, unabaki kwenye seat yako, ukiangalia nje unaona miti inakimbia. Mwendo wa dunia ni ule ule, haubadiliki.
 
Utalipita ila unahitaji kitu cha kukufanya uaccelerate zaidi ya speed uliyoko nayo kwenye gari , mathalani ujifunge rocket au spring ziwe attached kwenye gari na zikushoot way forward. First law of motion inasema vizuri. Its simple physics
 
Ni kwa sababu hatuna reference point labda ukienda anga za juu ukakae kwenye mwezi ndio utaona jinsi hiyo spidi ya maelfu ya kilomita inavyofanya kazi yake.
Lakini mkuu Satellite Iko nje ya Dunia (kile kituo Cha NASA kama sijapokea)
 
Lakini mkuu Satellite Iko nje ya Dunia (kile kituo Cha NASA kama sijapokea)
Yes iko nje, na ndiyo maana ni rahisi sana waliopo nje kuuona huo mzunguko wa dunia kila baada ya dakika kuliko sisi tulioko ndani ya dunia yenyewe.
 
Lakini mkuu Satellite Iko nje ya Dunia (kile kituo Cha NASA kama sijapokea)
Kile kituo kina mzunguko wake ila pia n kuzunguka dunia na ina spidi kuzidi speed ya dunia
 
Hakuna kitu kama hicho mjomba. Wazungu wanatupiga tu fix. Tungekuwa tunazunguka si tungeanguka kutokana na kizunguzungu.

Halafu si ndiyo hawa hawa wanaotudanganya eti zamani tulikuwa manyani kupitia ile theory yao ya Evolution of Man! Ukiwauliza siku hizi mbona hatubadiliki, hawana majibu!
 
Ni kama ukutane na mtu anayenuka mdomo alafu ujiulize hivi yeye hasikii anavyonuka?

Au upite maeneo ya Sinza, tandale na maneo ya dsm yanayonuka. Wakazi wa eneo lile hawasikii harufu kwa sababu wao ni sehemu ya hiyo harufu.
🤣🤣
 
Hakuna kitu kama hicho mjomba. Wazungu wanatupiga tu fix. Tungekuwa tunazunguka si tungeanguka kutokana na kizunguzungu.

Halafu si ndiyo hawa hawa wanaotudanganya eti zamani tulikuwa manyani kupitia ile theory yao ya Evolution of Man! Ukiwauliza siku hizi mbona hatubadiliki, hawana majibu!
Inafikirisha sana
 
Back
Top Bottom