Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Ukienda Dodoma, miradi mingi inatekelezwa na Kampuni ya Suma JKT. Na wanafanya miradi ile kwa kulipwa mabilioni ya fedha.
Wana Kampuni ya Maji ya Uhuru ambayo inatengeneza maji na kuuza kwa kiwango kikubwa sana. Kwenye shughuli karibu zote za Serikali maji yanayogawiwa ni ya Kiwanda cha Maji cha Suma JKT.
Wana Kampuni ya Ulinzi ambayo nayo inafanya vizuri kwa kupewa tenda za ulinzi katika ofisi za Serikali na Kampuni binafsi nchi nzima.
Wana Kampuni ya Kutengeneza Taa za Solar ambayo inafanya kazi vizuri sana.
Swali ni Je Kampuni hizi za Jeshi kwa nini Hazitoi Gawio kwa Serikali? Pesa zake zinaenda wapi?
Pia Msajili wa Hazina anazisimamia lweli hizi Kampuni? Kama majibu ni ndiyo taarifa zake za mapato na Matumizi ziko wapi?