Kwanini hatutumii treni kusafirisha mafuta?

Yanasafirishwa sema bahewa ni chache sana hazikidhi
 
Wanasafirisha bandugu ukienda hapo tanga tu mkwakwani utazikuta treni zinavuta matanka ya mafuta
 
Tunasubiria kuokota vichwa vya treni bandarini, unadhani tutaweza kununua matanki ya kusafirisha mafuta!?
Tutakaa tusubirie kuokota na matank!

Treni ni usafiri cheap, bahati mbaya reli zetu hazifiki maeneo mengi, na maeneo yenye uhitaji yamekuwa mengi na makubwa zaidi, halafu serikali ndiyo inang'ang'ania kuendesha biashara ya treni! Usimamizi mbovu! Ubadhirifu umetamalaki! Aaaagh, basi tu ndiyo Africa!
 
Kuwe na mtandao wa mabomba toka bandarini mpaka kila mkoa???
Hela za huo mtandao beberu yupi atatukopesha!?
Service Tu za pampu za maji Ziwa Victoria, wanategemea beberu! Behind the scenes, front utawasikia Sisi tunaweza, tumefanya, tunatekeleza blah blah!
 
Kwa reli ipi hiyo wakati railway network inapita mikoa kadhaa tu na mwendo wake wa konokono
 
Kwenda wapi? Mbona Malawi Cargo wanatoa mafuta Dar kwa treni hadi Iyunga Mbeya kwenye deport yao?
 
Sababu mashirika ya reli yamelala hayajui kuchangamkia fursa kama jamaa wa maroli
 
Tazara akabidhiwe Mchina, ya Kati apewe wa nje serikali ichukue tu posho yake, maana imefeli kuendesha
 
Miaka ya nyuma kabla ya ubinafsi (shaji) uliofanywa na Nzee Nkapa, mafuta yalikuwa yanasafirishwa kwa magusi
 
Halafu cha kusikitisha zaidi kila mwaka shirika la reli linapata hasara.
Nina uhakika hii miradi ya Reli angepewa mtu kama Bakhresa aiendeshe serikali ingepata pesa nyingi sana ya kodi na pia sisi wateja tungepata huduma bora na ya uhakika kuliko hivi sasa inavyoendeshwa na hawa wapigaji wa TRC.
 
Aina ya wabunge ndiyo hao kina Mbatia, COVID-19 wa mfano, wengine wapiga sarakasi, wengine wananunua kuitwa Dokta, tusitegemee makubwa!

Serikali ilishashindwa kufanya biashara iwe Tu shareholder, au iachie sector binafsi, yenyewe ikusanye Kodi na kupata magawio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…