Kwanini hautumii mtandao wa Facebook?

Kwanini hautumii mtandao wa Facebook?

Facebook naikubali kwa sababu watu wapo real yaani hakuna kufekifeki kwingi na kama mtu ukitaka kujua kitu flani , kule kuna group za kila aina na watu wanafunguka practically, achana na motivational speaking . Kingine kuna baadhi ya nchi zinatumia FB kuliko hata insta or tiktok kwa hiyo kule kwa groups za nje pia zipo vizuri lakini pia napenda, ipo simple kuitumia
 
Hello keyboard warriors,

Imekuwa kawaida sana kusikia kauli kama "Bado unatumia Facebook?" pale mtu anaposhika simu yako na kuikuta hiyo app.

Binafsi mtandao wangu pendwa wa muda wote ukitoa JamiiForums ni Facebook.

Kwanini wewe hutumii Facebook ilhali watu maarufu wote wanautumia na mnatuchukuliaje sisi tunautumia, na wale mnaotumia huo mtandao mnawachukuliaje ambao hawautumii?
Kila mtu apende kitu chake binafsi Mimi natumia Facebook muda mrefu Sana na sijapanga kuacha kabisa kwanza wanaosema bado unatumia Facebook Ni washamba kabisa

Mademu wengi nimewapata Facebook siwezi acha tumia Facebook
 
Hello keyboard warriors,

Imekuwa kawaida sana kusikia kauli kama "Bado unatumia Facebook?" pale mtu anaposhika simu yako na kuikuta hiyo app.

Binafsi mtandao wangu pendwa wa muda wote ukitoa JamiiForums ni Facebook.

Kwanini wewe hutumii Facebook ilhali wat maarufu wote wanautumia na mnatuchukuliaje sisi tunautumia, na wale mnaotumia huo mtandao mnawachukuliaje ambao hawautumii?
Facebook kwangu ni no moja kwanza rahisi kuperuzi, wanaosema ivo nawaona washamba tu Facebook inakuunganisha na watu uliopoteana nao kitambo hata kufanya biashara Facebook rahisi sana na wateja ni wengi ad raha.
 
Nilitumia 2009 hadi 2010,nikaacha nikahamia twitter badaye 2013 nikajiunga JF hata twitter naona kituko naingia Mara 2 kwa mwezi.

Huko Facebook,twitter,tik took,instagram ukiwa unafanya biashara ndio mahala pake,na ujinga jinga nao upo mwingi tofauti na JF.
 
Facebook Marketplace
Facebook ndio sehemu rahisi ya kuuza na kununua bidhaa "Market Place" kitu changu chochote nikitaka kuuza/kununua Ni FB mpaka hii simu nimununua kule hata kitu kiwe hakina thamani through FB utauza kwa urahisi.

GROUP
Kwa Group FB ipo vizuri Mimi nipo Group la Ajira za walimu Tamisemi na mengine ya Biashara, uzuri wake hata Sasa ukihitaji Group la kisevu purpose yako uki serch kule unalipata.

Pia kwenye Group unaweza post uka share Group nyingi na Engagement ya wateja kubwa kuliko WhatsApp.
 
Sababu za hao wapuuzi wanaouliza "bado unatumia Facebook?" Ni mbili tu;
1. Wengi wao wapo mitandaoni kwa ajili ya kuchat tu na kujiburudisha.
2. Na hata wale wanaofanya biashara wana upuuzi wa kudhani Facebook haina watu wengi kama Instagram na mitandao mingine. Wasichokijua ni kuwa bado Facebook ni mtandao unaoongoza kwa wafuasi. Na kama ni wateja basi Facebook inaongoza kwa kuwa na wateja wa uhakika. Madingi wengi wako Facebook.
Hapo kwa wateja wa uhakika Facebook nimekuelewa kufanya biashara Facebook utaenjoy.
 
S
Natumia toka 2011 tena nilifunguliaga akaunti internet cafe pale njia panda ya kuvuka Msewe kutokea Morogoro Road, sasa nitaanzia wapi kuiacha!
2010 nadhani nilifungua na simu ya mtu yenye internet nikasahau password nayotumia kwa Sasa nimefungua 2012
 
Facebook imenipa wanawake wengi Sana imagine hujawahi fika mkoa X na yeye hajawahi fika mkoa ulipo ila mme meet facebook after long chat mnaonana na kutengeneza familia daa
 
Situmii Mtandao wowote wa Kijamii zaidi ya JF tu
 
Back
Top Bottom