Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,771
- 14,129
Dkt Magufuli ilikuwa hulka yake kusikiliza kero kwa wananchi. Hata alipokuwa waziri, anapokuwa ofisini aliweza kutoka nje ya ofisi yake na kuwasililiza wananchi waliojitokeza na shida mbali mbali na kuzitatua hapo hapo. Unajua watanzania hatupendani, wewe ukitaka kujua hatupendani nenda kwa mkuu wa wilaya halafu sema una shida naye uone mlolongo wa ukiritimba utaopewa. Kwa ujumla viongozi Tanzania ni miungu watu, na ndiyo maana tunahitaji uongozi wa kizazi kipya ambacho kitasema tupunguze matumizi ya v8, tupunguze majimbo ya uchaguzi, balaza la mawaziri liwe na watu 12 tu etc. lakini sasa hivi viongozi watatumbua hela utadhani wanaenda shambaniWakuu salama…
Enzi za uhai wake, Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli alikuwa ni mpenda drama sana.
Angeweza kusafiri kwa gari kutoka Dodoma pengine kuelekea Chato.
Angeweza kufika Singida na kusimama barabarani bila kujali anasababisha foleni kwa walipa kodi wanaotumia barabara husika.
Angeanza kujigeuza hakimu kusikiliza mara mtu kadhulumiwa shamba lake, mara madarasa hayajajengwa, mara mke na mume wamegombana na kuachana.
Magufuli akawa anajigeuza hakimu na wakati mwingine jaji. Angeweza kutoa maamuzi na akapiga na mkwara mzito kwa wateule wake.
Kazi ya mahakama ikawa imeingiliwa na kuzibwa mdomo na Rais.
Mahakama kwanini ilikubali kuingiliwa uhuru wake wa utendaji kazi?