mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,707
Hakika nimeshangazwa na Uongozi wa Hospital ya Regency kutoza tozo la kumwona Daktari mara mbili kwa ugonjwa ule ule.Jana tarehe 6/9/2018 nilienda kutibiwa pale.Nikatimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na tozo la daktari.Daktari alinihudumia na kuniandikia vipimo ila akaniambia majibu nimpe kesho.Kweli nilishughulikia vipimo siku hiyo hiyo lakini ikabidi kesho yake nivipeleke.Kilichonishangaza ni kutakiwa kulipa tena tozo la kumwona Daktari.Swali langu kwani nilipe tozo mara mbili la kumwona Daktari huyo huyo aliyenisababisha nimwone kesho wakati angeweza kuvipata vipimo siku ile ile? Au kusema kesho ni mbinu ya kulipa tena?Wadau tushauriane.na uongozi utoe ufafanuzi.