KWANINI HOSPITAL YA REGENCY INATOZA TOZO LA KUMWONA DAKTARI MARA MBILI KWA UGONJWA ULE ULE?

KWANINI HOSPITAL YA REGENCY INATOZA TOZO LA KUMWONA DAKTARI MARA MBILI KWA UGONJWA ULE ULE?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika nimeshangazwa na Uongozi wa Hospital ya Regency kutoza tozo la kumwona Daktari mara mbili kwa ugonjwa ule ule.Jana tarehe 6/9/2018 nilienda kutibiwa pale.Nikatimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na tozo la daktari.Daktari alinihudumia na kuniandikia vipimo ila akaniambia majibu nimpe kesho.Kweli nilishughulikia vipimo siku hiyo hiyo lakini ikabidi kesho yake nivipeleke.Kilichonishangaza ni kutakiwa kulipa tena tozo la kumwona Daktari.Swali langu kwani nilipe tozo mara mbili la kumwona Daktari huyo huyo aliyenisababisha nimwone kesho wakati angeweza kuvipata vipimo siku ile ile? Au kusema kesho ni mbinu ya kulipa tena?Wadau tushauriane.na uongozi utoe ufafanuzi.
 
Uliwauliza hapo mapokezi wakakupa sababu za ww kutakiwa kulipia tena?!
 
Hiyo Regency ni private au hizi zetu za umma? Lkn pia ni vizuri ungewaeleza kuwa unarejea kwa mara ya pili, wangezingua hapo ni kuwaanzishia timbwili tu maana huo ni wizi.
 
Taratibu za clinic kwa hospital zote Tz ni kulipia kila unapomuona Daktari kwa siku haijalishi kama haujapona (consultation fees)

Suala la kukuambia ukapime vipimo tayari ilikuwa ni huduma tosha kwa maana ya consultancy ambapo lazima ukishapima usomewe icho kipimo so kwa vile ratiba ya siku hiyo tayari ilishabana ndio maana unaambiwa uje siku nyingine kwa ajili ya kusomewa icho kipimo na hapo itabidi ulipie tena

Nafikiri ulipofika hapo uliona huo wingi wa wagonjwa ambapo sio rahisi kwa wewe kwenda kupima na kurudi kukuta Dr bado anakusubiri
 
Hakika nimeshangazwa na Uongozi wa Hospital ya Regency kutoza tozo la kumwona Daktari mara mbili kwa ugonjwa ule ule.Jana tarehe 6/9/2018 nilienda kutibiwa pale.Nikatimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na tozo la daktari.Daktari alinihudumia na kuniandikia vipimo ila akaniambia majibu nimpe kesho.Kweli nilishughulikia vipimo siku hiyo hiyo lakini ikabidi kesho yake nivipeleke.Kilichonishangaza ni kutakiwa kulipa tena tozo la kumwona Daktari.Swali langu kwani nilipe tozo mara mbili la kumwona Daktari huyo huyo aliyenisababisha nimwone kesho wakati angeweza kuvipata vipimo siku ile ile? Au kusema kesho ni mbinu ya kulipa tena?Wadau tushauriane.na uongozi utoe ufafanuzi.
Hata Tanga Burhan Charitable dispensary wanafanya wizi huo huo! Ni mbinu za kupata fedha. Nenda kwenye NIHF!
 
Huo ni wizi usipodhibitiwa Wadaktari watakuwa wanatuandikia kipimo kimoja kimoja kila siku ili umwone ulipe tozo
 
Back
Top Bottom