Najiulizaga sana, ama wewe hujiulizagi?
Kwenye biashara ama mishe hio hio unayofanya miaka nenda rudi unaishia kupata hela yakula tu
Ila anakuja mtu moja wala hana uzoefu kiviile nahio biashara ama kazi
Ila kwamuda mfupi tu mambo yake yamenyooka
Matajiri wa jf mtuambie nimbinu mnazitumia kuchezesha hapo __kwamuda mfupi tu mtu kafungua kiduka kidogo dogo mara gafla tu limekua duka la jumla mara kashanza kujenga mara kashanunua gari mara mara tayari duka nikubwa kabisa anashusha mzigo kwa mafuso
Nawasilisha
nadhani mambo yanayofanya utoboz unakua mgumu ni pamoja na,
kutokua na dira malengo ya wazi, muda na vipaumbele muhimu vya kuzingatia na kuanza navyo..
vijana wanachagua sana kazi na vipaumbele mpaka jua linazama dah🐒
kukata tamaa haraka sana. vijana wengi hawataki hasara wala pressure bana, hawataki kujishughulisha na kupambana kabsaa..
wanataka faida tu.
hapo utoboz utausikia kwa wenzio tu..🐒
vijana wanaigiza sana maisha. ukimuona kijana wa leo utadhani ni bosi flani vile, kumbe ni kapuku tu. Atatoboaje apo hataki vumbi hataki jasho, anataka tu kunukia perfume vizur na kuskiza mziki mnene.
Hawez toboa aise 🐒
maisha ya kujilinganisha sana na wengine yamechelewesha wengi sana kutoboa, na hata walio toboa hawana shukran kabisa kwa Mungu na kwa walio wasaidia kutoboa, au walau basi na wao kua msaada wa kusaidia wengine nao watoboe.
Mungu ni wetu sote, yafaa sifa na shukrani ziende kwake ili baraka na Neema ziendelee kutumiminikia 🐒
karibuni shamba utoboz ni bwerere tu na wa uhakika. ni uvumilivu wako tu, ustahimilivu wako tu na subra 🐒