Kwanini hujatoboa mpaka leo?

nadhani mambo yanayofanya utoboz unakua mgumu ni pamoja na,

kutokua na dira malengo ya wazi, muda na vipaumbele muhimu vya kuzingatia na kuanza navyo..
vijana wanachagua sana kazi na vipaumbele mpaka jua linazama dah🐒

kukata tamaa haraka sana. vijana wengi hawataki hasara wala pressure bana, hawataki kujishughulisha na kupambana kabsaa..
wanataka faida tu.
hapo utoboz utausikia kwa wenzio tu..🐒

vijana wanaigiza sana maisha. ukimuona kijana wa leo utadhani ni bosi flani vile, kumbe ni kapuku tu. Atatoboaje apo hataki vumbi hataki jasho, anataka tu kunukia perfume vizur na kuskiza mziki mnene.
Hawez toboa aise 🐒

maisha ya kujilinganisha sana na wengine yamechelewesha wengi sana kutoboa, na hata walio toboa hawana shukran kabisa kwa Mungu na kwa walio wasaidia kutoboa, au walau basi na wao kua msaada wa kusaidia wengine nao watoboe.
Mungu ni wetu sote, yafaa sifa na shukrani ziende kwake ili baraka na Neema ziendelee kutumiminikia 🐒

karibuni shamba utoboz ni bwerere tu na wa uhakika. ni uvumilivu wako tu, ustahimilivu wako tu na subra 🐒
 
sawa lakini hunaweza kuthibitisha hili?
nishashudia bro zangu wanaanza hustle chini kabisa mbaka wanajipata unatak ni amini ni majambazi au wachawi ka unavyosema
pesa halali zipo ni kupambana tu
Wamejipata kwa level ipi?! Walivyokua makapuku walikua na nini, na sasahivi unavyosema wamejipata wana nini?

Nb: wakati mwingine watu hudanganya mengi sana nyuma ya hizi keyboard!! Kwaio sitashangaa ukiniambia kwa sasa wanamiliki Lexus LX ya Milioni 650.
 
Ridhika na ulichonacho mkuu.

Utajiri wote huu wa dunia unaona ni ubatili mtupu.
Maneno ya waliokata tamaa. Umaskini una njia ya kuharibu watu akili. Kwamba hio shilingi 500 uliyonayo unayosema umeridhika nayo, inaweza kumtibu mtoto wako akiumwa
 
Akili ya masikini Pumbavu
subiria mshahara wako wa afisa daraja la II mpaka siku ya kustaafu halafu ukafie mbele huko
Huna mchang wowote kwenye jamii zaidi ya kuomba rushwa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] akibahatika kufika miaka 50 ndio wale wanakaa vibarazani wanasubiri waondoke duniani.
 
Mkuu, ni bora kutokuchangia kuliko kuja na porojo za kukatisha watu tamaa bila ushahidi
Nimemzimisha ili watu wenye mchanga chanya walete miongozo, maana hizo porojo zake zinaweza kuuteka uzi wote ukapoteza maana
Umaskini umeharibu sana sana akili za walio wengi tanzania. Wako kama mazombie. Wewe si unawaona wamejazana kule kwa bulldoza na zumaridi wanaangalia live show michael jackson anavyofufuliwa
 
Maneno ya waliokata tamaa. Umaskini una njia ya kuharibu watu akili. Kwamba hio shilingi 500 uliyonayo unayosema umeridhika nayo, inaweza kumtibu mtoto wako akiumwa
Wanatafut utajiri mkuu sasa mbona unawaponda?
 
Kutoboa ni relative mkuu.

Bakharesa naye akiwa na kina Dangote au billgate au Elon anajiona hajatoboa.

Mwijaku akiwa pale Kisota kigamboni anajiona katoboa lakini akiwa na kina Meley Barabu au Salaaah anajiona mchumba tu.

Wewe hapo na kajumba Kako cha vyumba viwili huko uswahili kwenu matola na ka IST unajiona umetoboa lakini ukija Mbweni JKT ukakutana na mansion kama za kina Lugumi au Lukosi na parking Lot ina madungu kama yote utajiona haujatoboa.

Kwahiyo kutoboa inategemea na wewe mtazamo wako na ndiyo maana kila leo kina Elon wanazidi kuinvest tu wanaona kama bado hawajatosheka wakati hiyo hela aliyonayo hata asipofanya kazi anaweza kuuitumia hadi miaka 100 na isiishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…