Kwanini Ibrahnation anakuwa underrated?

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu niwe mkweli tu huyu kijana mziki anaweza sijawahi pata ona..

Ule uwezo wake wa kunata na beat yoyote kwa melody ile ile bila kushuka.. Ni kipaji tosha..

Sasa kwanini basi anakuwa underrated kiasi hiki.?

Yaani hata management Hana mpka leo..!
Mbona ana nyimbo nzuri sana
Ila hii solo aliyoshirikishwa na dj seven ndo balaa jingine aseeh
Nyimbo Kama.
Kubali.
Tabibu.
Nieleze.
Na hii iliofanya vizuri zaidi. Nilipize..

Kwanini basi hata management akose msanii mzuri Kama huyu??
Your browser is not able to display this video.
 
Sijawahi kumuelewa kiukweli na nikikuta watu wanamuongelea kuwa ana uwezo mkubwa ndo huwa sielewi kabsaa..

je, yupo vizuri vocally kuliko beka ibrozama au ana uandishi mkali kuliko marioo au hata ana aura ya kuuzika kuliko wasanii waliopo

Labda unisaidie kuuona huo uspesho wake mkuu
 
mtazame vizuri mkuu ni moja ya wasanii wanaojua ku perform live .
Labda anachokosa ni brand tu bc
 
Leo kijana umeongea point ibranation ni msanii mzuri Sana na ana kipaji kikubwa kuliko wasanii wengi wa bongo kwa wale wanafuatilia series ya kapuni ya maisha bongo ndani ya zikizDStv yeye ndo amefanya ile soundtrack ya hiyo series na ni bonge moja ya soundtrack ila soko la bongo linataka msanii awe very active kwenye kutoa kazi almost si chini ya ngoma 5 kwa mwaka mmoja.Tatizo kijana anatoa ngoma moja sometime 2 kwa mwaka mmoja kwa style hii lazima wabongo wakupotezee.Tatizo lingine ana jificha Sana ni adimu Sana kumuona kwenye media na niliwahi kumshauri kwenye Instagram yake mshauri wangu mpaka leo hajaufanyia kazi.

Jambo lingine Hana management active, management itakayo push mziki wake uende.jambo la mwisho kabisa jamaa sio hard worker kabisa ili nalo linachangia asifike mbali kimziki.Mziki wa bongo utakiwi kujua kuimba pekee unatakiwa ujiongeze zaidi.
 
Is not underrated but he is low key
 
mda mwingine kijana unakuwaga una akili
 
Huyu jamaa ni kama foby tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…