Kwanini iitwe Tanganyika law society na sio Tanzania law society?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Wakuu kwa Sasa masikio yote yapo Dodoma kwenye mkutano wa mawakili na katika mkutano huo umefanyika uchaguzi ambao matokeo yake yanasubiriwa kwa hamu sana.
Maswali yangu kwa wajuzi:

1.Kwanini hii inaitwa Tanganyika law society na sio Tanzania law society??
2. Je Zanzibar napo huwa kuna Zanzibar law society??
3. Kuna wakati ndugu Fatma Karume kutoka Tanzania visiwani alokuwa mwenyekiti wa Tanganyika law society, je bila shaka hii ni kumaanisha hata mawakili kutoka Zanzibar ni wanachama na ndo MAANA bi Fatma alipata nafasi ya uongozi?

4. If that is the case, kwanini sasa haibadilishwi jina ikaitwa Tanzania law society Ili kumaanisha ni jumuiya ya mawakili pande zote mbili bara na visiwani?

Ngaiwoye
 
Kwanini Sasa ni Fatuma ambae anatokea Zanzibar alikuwa mwenyekiti wa Tanganyika law society na sio huko Zanzibar?
Uanachama wa TLS sio tu kwa ajili ya Watanganyika. Mtu yeyote kutoka nchi yoyote anayekidhi vigezo vya kuwa wakili kwa mujibu wa sheria anaweza kuwa wakili ndani ya Tanzania Bara (Tanganyika). Akishakuwa wakili hapa Tanganyika moja kwa moja anakuwa mwanachama wa TLS bila kujali uraia wake. Uanachama wa TLS unampa haki ya kugombea uongozi ndani ya TLS.
 
Una Miaka Mingapi??

Vyama Vingi vya Kitaaluma Vilianzishwa Kabla ya Muungano Ikiwemo TLS..
Na hata Chama Cha Madaktari Tanganyika..

Medical Council of Tanganyika..(MCT)..

KILA NCHI INA VYAMA VYAKE VYA KITAALUMA KWA SABABU SIO SWALA LA MUUNGANO HILO
 
Kwanini Sasa ni Fatuma ambae anatokea Zanzibar alikuwa mwenyekiti wa Tanganyika law society na sio huko Zanzibar?
Mzanzibari ni mtanganyika ila Mtanganyika siyo mzanzibari kwa kuwa Tanzania ni Tanganyika yenye Zanzibar ndani.
Kwa wale wanaofahamu nadharia ya seti, kati ya Tanzania na Zanzibar ipi ni universal set, au kati ya Tanganyika na Zanzibar ipi ni improper subset ya mwenzake?
Hii ni kwa ajili ya fikra huru tu, usielekeze kwenye siasa na mamlaka.
 
Uanachama wa TLS sio tu kwa ajili ya Watanganyika. Mtu yeyote kutoka nchi yoyote anayekidhi vigezo vya kuwa wakili kwa mujibu wa sheria anaweza kuwa wakili ndani ya Tanzania Bara (Tanganyika). Akishakuwa wakili hapa Tanganyika moja kwa moja anakuwa mwanachama wa TLS bila kujali uraia wake. Uanachama wa TLS unampa haki ya kugombea uongozi ndani ya TLS.
Mnaposema Tanzania bara halafu kule Tanzania visiwani mnaita Zanzibar mm siwaelewi. Kwa nn msiite huku Tanganyika na kule Zanzibar au huku Tanzania bara na kule Tanzania visiwani? TLS na hili NENDENI MKALISIMAMIE
 
Ni wewe tu kuamua uende kusoma Law school ya Tanganyika au Zanzibar.

Kama ukisoma Law school ya Tanganyika basi utajoin TLS na ukitaka kwenda Zanzibar kuna utaratibu unaufuata na unakuwa mwanachama wa kule.

Ukisoma Zanzibar ili uwe wakili Tanganyika lazima uwe ume-practice kwa miaka 5 Zanzibar ndipo unapoweza kuomba kusajiriwa pia Tanganyika (TLS).

Kama hujaelewa karibu uulize tena kesho nikimaliza kujipongeza kwa ushindi wa Mwabukusi
 
Kwa sababu tumewapa kazi maalum ya kuturudishia Tanganyika yetu!.

R.I.P MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA.
 
1.Kwanini hii inaitwa Tanganyika law society na sio Tanzania law society??
2. Je Zanzibar napo huwa kuna Zanzibar law society??
3. Kuna wakati ndugu Fatma Karume kutoka Tanzania visiwani alokuwa mwenyekiti wa Tanganyika law society, je bila shaka hii ni kumaanisha hata mawakili kutoka Zanzibar ni wanachama na ndo MAANA bi Fatma alipata nafasi ya uongozi?
Wana huo muda? Taarabu wataimba saa ngapi
 
Mnaposema Tanzania bara halafu kule Tanzania visiwani mnaita Zanzibar mm siwaelewi. Kwa nn msiite huku Tanganyika na kule Zanzibar au huku Tanzania bara na kule Tanzania visiwani? TLS na hili NENDENI MKALISIMAMIE
Katiba na sheria zetu zinatumia neno Tanzania Bara kuitaja hii sehemu ya muungano. Hazitumii neno Tanganyika.
 
Pia kuna kampuni yangu Tanganyika hospitality management company
Nazungumzia jumuiya ya wanasheria wa Tanganyika, ambayo Ina wanachama kutoka Bara na visiwani..kwanini isibadilishwe jina iitwe Tanzania law society?
 
Back
Top Bottom