Kama Kenya walipewa hayo masharti how did they get to this point?
Kenya walikopa madeni makubwa kutoka China wakashindwa kulipa,ndipo wakaigeukia IMF na World Bank kuomba mikopo zaidi ili wapunguze deni la China.Kama kawaida IMF na World Bank wakawapa "msaafu"wa masharti kibao,nasikia na ile Financial Bill ilitungwa na IMF. Matokeo ndio haya.
Kwetu baada ya vita vya Kagera hao IMF na World Bank walitupa masharti magumu lakini Raisi wakati ule Mwalimu Nyerere aliyakataa kata kata.
Lakini IMF na World Bank walimuona Mwalimu kama msaliti aliyekuwa ana ushawishi mkubwa kwenye nchi nyingi hasa dunia ya tatu,wakamtengenezea vimeo ili wamkwamishe kwa kila aina.
Kweli Mwalimu alipambana lakini ngoma ilikuwa nzito akaona heri aachie ngazi ya uraisi.
Yawezekana kwa sasa wako darling wa Tanzania kwani wanajua investment kubwa za madini,gesi asilia, chuma,mkaa wa Mawe,Madini ya Nickle huko Kabanga,Gesi ya Helium huko Sumbawanga,Madini ya Uranium,Graphite,Migodi ya Dhahabu,Tanzania kuzunguka nchi nyingi na miradi kibao ya miundo mbinu ya Umeme, Barabara,Reli,Meli wanajua kuna siku huyo Tanzania atapasua nao watapata maokoto.
Usishangae IMF na World Bank wakailegezea masharti Tanzania kwa makusudi na kumpa mihela kibao ili Kenya waone wivu ili wasalimu amri.