Kwanini inashauriwa kubadili Mafuta ya Brake kila baada ya miaka 2 au 48,000 Km?

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Ukienda kufanya service ya brake huwa unarekebisha au kubadili nini?

Je, umewahi kubadili Brake fluid?

Inashauriwa kubadili Brake fluid kila baada ya miaka 2 au 48,000Km (Lolote litaloanza kati ya hayo mawili) kwa sababu kuu mbili,

1. Kuingia kwa vumbi na particles zingine kwenye master cylinder kunaweza kuathiri ufanyaji kazi wa mafuta ya brake. Hili tuliache

2. Mafuta ya brake yana tabia ya kufyonza unyevu kutoka kwenye hewa. Ndio maana haishauri kuacha mfuniko wa master cylinder wazi. Hili la unyevu ndio hasa maada kuu.

Ingawa mfuniko wa master wa master cylinder muda mwingi unakuwa umefungwa, huwa kunakuwa na tundu dogo kwenye mfuniko kwa ajili ya kupumua (Breather). Hapa ndio unyevu huingia kwenye Brake fluid.

Asilimia ya kiasi cha unyevu kitakachokuwepo kwenye mafuta ya brake ndio itakayotuambia kama mafuta hayo yanafaa kuendelea kutumika au lah.

Mchanganuo upo kama ifuatavyo.

0% - 2% ya unyevu, Ni kiwango kinachokubalika.

3% ya unyevu, Tunashauri mtu abadilishe brake fluid.

Kuanzia 4% ya unyevu na kuendelea, Utahitajika kubadilisha mafuta ya brake haraka sana. Upo hatarini brake zako kufeli.

Tunacho kifaa maalumu kwa ajili ya kupima kiwango cha unyevu katika mafuta ya brake. Gharama ni Tsh. 10,000/= Kwa gari yoyote. Asilimia zaidi ya 95 ya gari ndogo zinazotembea humu barabarani zinatumia mafuta kwenye brake.

Pia kwa mtu atakayehitaji kumwaga mafuta ya brake tunayo tool ya kisasa ambayo hucommand pump ya ABS pamoja na solenoid valves za tairi na mafuta yote yakatoka kwenye mfumo.

Hii ni njia ya kisasa zaidi kwa sababu mafuta yote hutoka ukilinganisha na ile njia ambayo wengi hutumia (Kufungua bleed valve na kukanyaga Brake pedal, Hii huacha mafuta kwenye mfumo wa ABS kwa sababu pump haizunguki).

Pia baada ya kuweka mafuta mapya tutakufanyia ABS bleeding kwa mashine yaani kutoa hewa kwenye mfumo wa ABS. Na kwa gari za ulaya/marekani ukifanya ABS bleeding unakuwa ndio umeshamaliza kutoa hewa kwenye mfumo wote wa brake ila kwa gari za japan bado tutalazimika kutoa upepo kwa ya kawaida hata baada ya kufanya ABS bleeding. (Haya tunaweza kuzungumza gharama).


Pia

Kama unahitaji Diagnosis ya gari lolote dogo kampuni yoyote.

Unahitaji check up ya mifumo ya umeme. Charging system, Starting system, Battery n.k. Tuna kifaa maalumu kwa ajili ya kazi hii.

Unasikia kelele yoyote kwenye engine. Tinacho kifaa maalumu kutuambia kelele zinatokea sehemu gani exact.

Tuwasiliane

Nipo Dar es salaam, Magomeni, Mwembechai.

Simu/WhatsApp +255 621 221 606.

Karibuni sana.
 
how kwa wanaotumia perfomance breaks like brembos au cusco brands?

Kama hiyo brake system inatumia Dot 3 mpaka Dot 5 ya brake fluid. Hii inawahusu. Regardless ni brake ya namna gani.
 
Mkuu JituMirabaMinne hili swali nilikuwa najiuliza Sana kuhusu ubadilishaji wa brake fluid..
gari Yangu inaenda mwaka sasa tokea niagize na mafuta ya brake yako vilevile hayaishi na sijawahi kuongeza,sasa Kwa hili somo lako nimepata kitu na jumatatu ijayo nitakuja magomeni mwembechai kukuona.

asante Sana
 
Pia

Kama unahitaji Diagnosis ya gari lolote dogo kampuni yoyote.

Unahitaji check up ya mifumo ya umeme. Charging system, Starting system, Battery n.k. Tuna kifaa maalumu kwa ajili ya kazi hii.

Unasikia kelele yoyote kwenye engine. Tinacho kifaa maalumu kutuambia kelele zinatokea sehemu gani exact.

Tuwasiliane
 

Okay mkuu karibu sana.
 
Ukaona na comment yao uandikie 'Marker pen' kabisa maana sisi wengine tunaotumia speedo hapa mwandiko wetu hausomwi.... Mwe mwe mwe......
 
Shida inakuja kwenye ubora wa hicho utakachokuja kubadilisha.
Linapokuja kwenye swala la ubora , Tbs wamefeli vibaya mno kuna lubes ma liquors kibao counterfeit sokoni ,
Unaweza kuta unabadilisha brake fluid kwa nia njema kabisa halafu ukakuta unaharibu gari kwa products za low quality.
 


Watu wanachakachua kitu ambacho kina demand kubwa ndio maana katika lubes zote engine oil zinaongoza kwa kuchakachuliwa.

Next month nitakuwa nimeshapata tool moja kwa ajili ya kupima quality ya engine oil.

Brake fluid zinachoka kwa sababu ya contamination ya particles unyevu plus joto unapokanyaga brake pedal as ile fluid inapokuwa compressed inazalisha joto.

Watu wengi akishaanza kukosa brake ataenda kubadili raba za master cylinder ambapo automatically atawekewa oil nyingine.
 
Just make sure unapata oil analyzer ya uhakika na latest inayoweza kupima oil content, huwa inasaidia kujua hali ya ndani ya engine bila kufungua components
Mfano kama main na con bearings zimechimba ,shaba huingia kwenye oil, , ukiwa na oil analyzer unaweza kujua hilo bila hata kufungua kitu , very useful unapokagua gari za kununua mkononi au yard
 
Hicho kitu nimewaza Sana ndiyo maana nilikuwa mwoga kubadilisha
 
Hicho kitu nimewaza Sana ndiyo maana nilikuwa mwoga kubadilisha
Nilikuwa nataka kubadilisha geabox oil , kwenye gari flan , service history yake inasoma ilibadilishwa oil hiyo last 200k km, huko ulaya kabla haijafika Africa ,
tulinunua zile top names za oil , sitataja majina yake, ila tulikuwa na option ya gear oil kama nne hivi , majina makubwa makubwa unayoyajua , cha kusikitisha tulipopima viscosity ile oil ambayo imaekuja na gari na imetembea km laki mbili plus , bado ilionekana ni bora kushinda hizi mpya za bongo.ilibidi niamue kutofanya service hiyo hadi nitakapopata oil nzuri ikiwezekana hata kwa kuagiza nje
 

Upo sahihi mkuu.
 

I thought hii ishu iko kwenye oils peke yake kwa sehemu kubwa hasa engine oil na gearbox Oil ila nimekutana na kitu asubuhi hii kimenishtua kidogo.

Among gadgets ambazo ninazo, nina battery tester ambayo inanisaidia kupima vitu vingi mfano Hali ya battery, Charging, system, starting system, loading test n.k.

Sasa nimejaribu kupima battery ya gari ambayo ilinunuliwa ikiwa mpya kabisa kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja. Ni battery ya kampuni ambayo ina jina kubwa tu. Na hili ndio hasa limenishtua.

Aiseee nimekuta battery health iko moderate. Nimeona nmechoka. Nikajiuliza battery ambayo hata mwezi haijamaliza inakuwaje na battery health ambayo ni moderate?

I have decided to do some research kwenye hizi Car batteries. Siku za mbeleni nitakuja na majibu.
 

Pia nikipata hiyo engine oil tester inaweza kunisaidia kuidentify vitu vingi. Kuna vitu naweza nikajifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…