Injiri ya Barnaba Sio Injiri ya Kristo na haiendani na Theolojia ya Kristo hivyo haina mashiko kwa Wakristo.
Machache kati ya hayo ni kwamba.
-Mwandishi wake alikuwa na uelewa mdogo sana kuhusu jiografia ya Upalestina.
-Katika sura ya 99:21 mwandishi anaeleza alipanda kwa miguu kuelekea kijiji cha Kapernaumu, wakati kijiji hicho kipo zaidi ya mita 200 chini ya usawa wa bahari.
-katika sura ya 100 mwandishi anaeleza kuwa Yesu Kristo alienda Nazareti kwa mashua wakati kijiji hicho kipo mita 500 juu ya usawa wa bahari,
-Katika sura ya 151 anasema pia kuwa Yesu alienda Yerusalemu kwa mashua ukiangalia ramani inapingana na huo usemi.
-Barnaba ndiye pekee aliyeandika kuwa Mamajusi waliompelekea zawadi mtoto Yesu, walikuwa watu watatu tu, tofauti na Injiri ya Yesu ambayo haijataja idadi ya Mamajusi bali imetaja idadi ya zawadi tatu walizopeleka (uvumba, manemane na dhahabu)
-Katika sura 40:41 Barnaba analitaja jina la tunda la mti wa mema na mabaya kuwa ni tunda la Tofaa, lile alilokula Hawa ktk bustani ya Edeni, wakati kitabu cha mwanzo na Biblia kwa ujumla ambayo ndiyo chanzo pekee cha habari hii, haijataja popote jina la tunda la Tufaa ktk maelezo yake.
-Katika sura ya 54 Barnaba ameitaja Dinari kuwa ina Minuti 60, bila kujua kuwa Minuti ilikuwa fedha ya Uhispania iliyoanza kutumika mwaka 685 baada ya Kristo wakati wa utawala wa Khalifa Abdul Malaki. Enzi za Yesu hiyo fedha haikuwepo.
- Katika sura ya 150 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo alizaliwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato akiwa kiongozi, wakati ukweli ni kwamba utawala wa Pilato ulianza mwaka 26 na 27 baada ya Kristo kuzaliwa.
-Katika sura ya 97 Barnaba anamtaja Mtume Muhammad kuwa ni Masihi na Yesu anamwita Kristo bila kujua kuwa neno Kristo ni kwa Kigiriki na Masihi ni kwa Kiebrania yakiwa na maana moja.
-Katika sura ya 222 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo hakusulubiwa, aliondolewa na Malaika, kisha Yuda alisulubiwa badala yake.
-Katika sura ya 44 Barnaba anaeleza kuwa Ibrahimu alimtoa Ishmaeli awe sadaka katika madhabahu, na anamwita Mungu wa Ibrahimu, Ishmaeli na Yakobo, tofauti kabisa na Mwanzo 22.
-Katika sura ya 192 Barnaba anasema Mwishmaeli ndiye aliyeiandika Torati.
-Barnaba anamweka mtume Muhammadi kama mbadala wa Yesu kristo, angalia sura ya 44, 45, 9, 112, 39 na nyinginezo ktk kitabu hicho.
{ hii ndiyo injili mnayoipigania iwekwe kwenye Biblia takatifu ? }
Katika ukweli huu mchache nadhani wasomaji mmeelewa mlengo wa Injiri ya Barnaba wala sina haja ya kuwaambia.
Injiri iliyowekwa katika biblia inaeleza wazo moja (maudhui yanafanana) ingawa inatofautiana maneno kutokana na mazingira ya kila mwandishi alivyofunuliwa na Yesu mwenyewe, tofauti na Injiri ya Barnaba.
[ Ndio maana kuna msemaji mmoja hapo juu nimemwambia, kama anaihitaji Injiri ya Barnaba, inapatikana madukani, akainunue na kuitumia ]
Hapo zamani za kale, kuna mtume mmoja alitokewa na kiumbe asichokijua, kwenye pango, na bila ya kujitambulisha kwamba kiumbe hicho ni kiumbe gani. Ghafla kikamkaba Koo na kumwambia " SOMA "