Kwanini injili ya Barnabas iliteketezwa?

Dunia tunayoishi sasa hivi sio hiyo unayoongelea. Tunataka kujua ukweli wa mambo.

Kwanini jambo fulani lilifanyika hivi na si vile? Kwanini fulani na si fulani?

Tunataka kuujua ukweli hayao mambo ya kusema imani yamepitwa na wakati.
Unachosema ni kweli ila je ni akina nani hao wanaopaswa kujibu haya yanayohojiwa? kwa sababu nimefuatilia sana hoja kama hizi ila naona watu wakiishia kutoa mitazamo yao tu.
 
Mkuu inaweza ikawa Sio hoja kwakua biblia vitabu vingi vya biblia havikuandikwa kipindi kile kile ambacho hao manabii wapo....Ila inaweza ikawa hoja kulingana na muktadha tunaoupata katika kitabu Cha injili ya barnaba ambayo imekuja kugunduliwa imeghushiwa ivyo tunaweza tukajenga hoja kwamba Kuna vitabu vingine viliandikwa na wapinga Imani kwa ajili ya faida yao.... na upotoshaji ulianza toka zamani
 
Kwa hali hii ni ngumu hata kupambanisha biblia na vitabu vyengine ili kutaka kujua ni kipi kitabu cha kweli.
Mkuu Biblia ni compilation tu sema nachotaka tuelewane ni kwamba hakukuwa na standard biblia kabla ya AD 382 ila vilikuwepo tu vitabu vya manabii mbalimbali sasa unaposema BIBLIA na vitabu vingine una maana gani?? Ilihali vyote viliandikwa muda mmoja ila tu havikuchaguliwa na Wakatoliki wa council of Rome

So tusiitaje BIBLE kana kwamba ilikuwepo tokea Yesu akiwepo bali tuongelee vitabu kama vitabu...mfano Gospel of Barnabas vs Gospel of Luke n.k ila isiwe Gospel of Barnabas vs BIBLIA NZIMA..... Sio ulinganisho sahihi mkuu
 
Imeghushiwa kivipi?? Mbona hata wanatheolojia wameconclude kuwa barua za paulo almost 5 ni discontented letters ikimaanisha ni Pseudepigrapha na sio maandishi halisi ya paulo lakini mbona kwenye Bible havijatolewa??

Nafikiri sababu ya kitabu cha Barnabas kutokuwekwa ni content yake kwamba inakinzana na maandiko mengine ya kama Injili ya luka,Yohana n.k ila kusema ni forgery sidhani kama ina mashiko maana kuna vitabu zaidi ya 12 vya Biblia ambavyo vina sura ambazo zimeandikwa miaka mingi baada ya original manuscripts kuwa zimeshaandaliwa mfano kitabu cha isaya na Jeremiah ila sijasikia hoja ikiibuliwa kuwa vifutwe kwenye Biblia.

Hivyo tusifanye selective judgement mkuu
 
Injiri ya Barnaba Sio Injiri ya Kristo na haiendani na Theolojia ya Kristo hivyo haina mashiko kwa Wakristo.
Machache kati ya hayo ni kwamba.
-Mwandishi wake alikuwa na uelewa mdogo sana kuhusu jiografia ya Upalestina.
-Katika sura ya 99:21 mwandishi anaeleza alipanda kwa miguu kuelekea kijiji cha Kapernaumu, wakati kijiji hicho kipo zaidi ya mita 200 chini ya usawa wa bahari.
-katika sura ya 100 mwandishi anaeleza kuwa Yesu Kristo alienda Nazareti kwa mashua wakati kijiji hicho kipo mita 500 juu ya usawa wa bahari,
-Katika sura ya 151 anasema pia kuwa Yesu alienda Yerusalemu kwa mashua ukiangalia ramani inapingana na huo usemi.
-Barnaba ndiye pekee aliyeandika kuwa Mamajusi waliompelekea zawadi mtoto Yesu, walikuwa watu watatu tu, tofauti na Injiri ya Yesu ambayo haijataja idadi ya Mamajusi bali imetaja idadi ya zawadi tatu walizopeleka (uvumba, manemane na dhahabu)
-Katika sura 40:41 Barnaba analitaja jina la tunda la mti wa mema na mabaya kuwa ni tunda la Tofaa, lile alilokula Hawa ktk bustani ya Edeni, wakati kitabu cha mwanzo na Biblia kwa ujumla ambayo ndiyo chanzo pekee cha habari hii, haijataja popote jina la tunda la Tufaa ktk maelezo yake.
-Katika sura ya 54 Barnaba ameitaja Dinari kuwa ina Minuti 60, bila kujua kuwa Minuti ilikuwa fedha ya Uhispania iliyoanza kutumika mwaka 685 baada ya Kristo wakati wa utawala wa Khalifa Abdul Malaki. Enzi za Yesu hiyo fedha haikuwepo.
- Katika sura ya 150 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo alizaliwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato akiwa kiongozi, wakati ukweli ni kwamba utawala wa Pilato ulianza mwaka 26 na 27 baada ya Kristo kuzaliwa.
-Katika sura ya 97 Barnaba anamtaja Mtume Muhammad kuwa ni Masihi na Yesu anamwita Kristo bila kujua kuwa neno Kristo ni kwa Kigiriki na Masihi ni kwa Kiebrania yakiwa na maana moja.
-Katika sura ya 222 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo hakusulubiwa, aliondolewa na Malaika, kisha Yuda alisulubiwa badala yake.
-Katika sura ya 44 Barnaba anaeleza kuwa Ibrahimu alimtoa Ishmaeli awe sadaka katika madhabahu, na anamwita Mungu wa Ibrahimu, Ishmaeli na Yakobo, tofauti kabisa na Mwanzo 22.
-Katika sura ya 192 Barnaba anasema Mwishmaeli ndiye aliyeiandika Torati.
-Barnaba anamweka mtume Muhammadi kama mbadala wa Yesu kristo, angalia sura ya 44, 45, 9, 112, 39 na nyinginezo ktk kitabu hicho.
{ hii ndiyo injili mnayoipigania iwekwe kwenye Biblia takatifu ? }
Katika ukweli huu mchache nadhani wasomaji mmeelewa mlengo wa Injiri ya Barnaba wala sina haja ya kuwaambia.
Injiri iliyowekwa katika biblia inaeleza wazo moja (maudhui yanafanana) ingawa inatofautiana maneno kutokana na mazingira ya kila mwandishi alivyofunuliwa na Yesu mwenyewe, tofauti na Injiri ya Barnaba.
[ Ndio maana kuna msemaji mmoja hapo juu nimemwambia, kama anaihitaji Injiri ya Barnaba, inapatikana madukani, akainunue na kuitumia ]

Hapo zamani za kale, kuna mtume mmoja alitokewa na kiumbe asichokijua, kwenye pango, na bila ya kujitambulisha kwamba kiumbe hicho ni kiumbe gani. Ghafla kikamkaba Koo na kumwambia " SOMA "
 
Ulichokisema ndiyo nilichokuwa nakiwaza mimi,nilikuwa nakumbushia kwenye ule uzi wako mwengine uliponiuliza ni kipi kitabu cha kweli?maana hizi dini tatu kila mmoja hudai kitabu chako ndiyo cha kweli.
 
Ulichokisema ndiyo nilichokuwa nakiwaza mimi,nilikuwa nakumbushia kwenye ule uzi wako mwengine uliponiuliza ni kipi kitabu cha kweli?maana hizi dini tatu kila mmoja hudai kitabu chako ndiyo cha kweli.
...werevu tunahitimisha kuwa vitabu vyote ni vya kutungwa na binadamu,_hivyo hakuna haja ya kuviamini kama vitukufu Mara sijui vitakatifu
....ingawa vinafaa kwa mafundisho ya kijamii
 
Ila injili ya barnaba haiendani kabisa na theolojia ya kikristo...mwandishi yule anaejiita barnaba alishindwa kuficha hisia zake dhidi ya ukristo
 
Great input.
Barikiwa
 
...werevu tunahitimisha kuwa vitabu vyote ni vya kutungwa na binadamu,_hivyo hakuna haja ya kuviamini kama vitukufu Mara sijui vitakatifu
....ingawa vinafaa kwa mafundisho ya kijamii
Hilo hitimisho ni la kivivu mkuu,hata kama hivyo vitabu viwe na makosa lakini kuhitimisha kuwa vimetungwa tu na watu mwanzo mwisho ni jambo ambalo haliniingii akilini.

Hivyo vitabu kuna baadhi ya vitu ambavyo vimeelezwa humo huwezi kusema kama hao waliyokuwa wakielezwa kipindi hicho kwamba walikuwa wanayaelewa,kuna mambo mengi yamekuja kufafanuliwa na kueleweka zama hizi. Sasa ikiwa watu walitunga tu ili wapate waumini,wasingejisumbua kuandika mambo mengi na mengine yasiyoeleweka kipindi hicho.
 
Neno walahi
 
Nani alikuwa na mamlaka ya kuikataa injili ya barnaba? halafu kama hoja ni hizo mbona tofauti zipo hata kwa kina MATHAYO, Marko na yohana lakini hamkuvifuta kama hoja ni kutofautiana
 
Nani kaghushi ? unaweza kuthibitisha angalau andiko moja ambalo wewe unahisi limeghushiwa kwadalili zilizo wazi
 
Injiri ya Barnabas haijateketezwa na ipo mitaani inauzwa na wala haijapigwa marufuku na taasisi yoyote, kama kitabu cha Aya za Shetani.
Kama unaihitaji unaweza kuinunua na ukaisoma na kuifuata bila bigudha yoyote ile kama unaipenda.
Alietunga kitabu cha aya za shetani nayeye alikuwa swahaba wa mtume? Vip barnaba alikuwa ni nani kwa Yesu? naona unajaribu kulinganisha visivyo kuwepo komaa kwenye mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…