Kwanini intaneti isiwe bure?

Kwanini intaneti isiwe bure?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wanasema tupo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda. Hayo yanategemea sana internet.

Kwa hiyo kwa sasa internet ni kama barabara kwa umuhimu wake.

Upatikanaji wa internet unawezesha maelfu ya shughuli za kiuchumi kufanyika.

Sasa ili kukuza huo uchumi kwanini serikali hazifanyi/haifanyi internet kuwa huduma ya bure?

Maana internet tunayotumia inatokana na mkongo wa Taifa ambao umejengwa na Serikali.

Mnaonaje internet ikawa bure?
 
Wanasema tupo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda. Hayo yanategemea sana internet. kwa hiyo kwa sasa internet ni kama barabara kwa umuhimu wake. Upatikanaji wa internet unawezesha maelfu ya shughuli za kiuchumi kufanyika. Sasa ili kukuza huo uchumi kwanini serikali hazifanyi/haifanyi internet kuwa huduma ya bure? Maana internet tunayotumia inatokana na mkongo wa taifa ambao umejengwa na serikali.

Mnaonaje internet ikawa bure?

Internet inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye miundo mbinu kuifanya kufanya kazi. Yahitaji watu kuhakikisha inafanya kazi.

Yahitaji umeme, masafa (frequencies) na bado TOZO pendwa za kizalendo tokea kwake bwana Madelu.

Inakuwa vipi bure hapo mkuu?
 
Wanasema tupo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda. Hayo yanategemea sana internet. kwa hiyo kwa sasa internet ni kama barabara kwa umuhimu wake. Upatikanaji wa internet unawezesha maelfu ya shughuli za kiuchumi kufanyika. Sasa ili kukuza huo uchumi kwanini serikali hazifanyi/haifanyi internet kuwa huduma ya bure? Maana internet tunayotumia inatokana na mkongo wa taifa ambao umejengwa na serikali.

Mnaonaje internet ikawa bure?

Inawezekana..
Hatujapata Viongozi serious..

Free with fi inatakiwa kila mji..

Na serikali irushe satellite yake ..

Rwanda Wana satellite 9..
Sisi hata moja Tu ya kwetu inatushinda..
 
Wanasema tupo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda. Hayo yanategemea sana internet.

Kwa hiyo kwa sasa internet ni kama barabara kwa umuhimu wake.

Upatikanaji wa internet unawezesha maelfu ya shughuli za kiuchumi kufanyika.

Sasa ili kukuza huo uchumi kwanini serikali hazifanyi/haifanyi internet kuwa huduma ya bure?

Maana internet tunayotumia inatokana na mkongo wa Taifa ambao umejengwa na Serikali.

Mnaonaje internet ikawa bure?
Wenye miundombinu watalipwaje, maana ama utumie internet via fibre optics ama satelite kama Stalink ya bwana Elon Musk. Yote hayo yanahitaji pesa kutengeneza, kutunza na kuendelea uvumbuzi na kusambaza huduma.
 
Wenye miundombinu watalipwaje, maana ama utumie internet via fibere optics ama satelite kama Stalink ya bwana Elon Musk. Yote hayo yanahitaji pesa kutengeneza, kutunza na kuendelea uvumbuzi na kusambaza huduma.
Hii internet ya mkongo si miundombinu ni ya serikali. Ifanye kama ilivyo barabara serikali inagharamia lakini zinarahisisha shughuli za uchumi. Tungekuwa na interent ya bure, serikali ingeweza kupata pesa nyingi kuliko ilizowekeza. Tungekuwa na netflix yetu na serikali ingepiga kodi humo, kwa ujumla kungekuwa na streaming services nyingi sana ambazo serikali ingepiga pesa kupitia kodi. Hapo bado biashara na huduma za mitandaoni, elimu ya online, afya, vyuo nk. Mwalimu anafundisha online, daktari anafanya consultation online, mwanasheria anaonana na mteja online nk.
Internet ya bure inaweza fungua mambo na ubunifu wa kushangaza sana kwenye uchumi.
 
Internet inhitaji uwekezaji mkubwa kwenye miundo mbinu kuifanya kufanya kazi. Yahitaji watu kuhakikisha inafanya kazi.

Yahitaji umeme, masafa (frequencies) na bado TOZO pendwa za kizalendo tokea kwake bwana Madelu.

Inakuwa vipi bure hapo mkuu?
Ni keeli gharama za mwanzo ni kubwa, lakini hata barabara zina gharama kubwa lakini tunatumia bure sababu zinarahisisha shughuli za kiuchumi.
 
Naunga mkono hoja

#lakini hilo haliwezekani[emoji18]#
Inawezekana. Tena indirect return yake inaweza kuwa kubwa kuzidi uwekezaji. Tunaweza kuwa nchi ya kwanza kutoa internet bure. Yaani internet inakuwa ni sehemu ya mahitaji muhimu ya binadamu. Na dunia ndiko inakoelekea, internet itakuwa sehemu ya mahitaji ya binadamu.
 
Wanasema tupo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda. Hayo yanategemea sana internet.

Kwa hiyo kwa sasa internet ni kama barabara kwa umuhimu wake.

Upatikanaji wa internet unawezesha maelfu ya shughuli za kiuchumi kufanyika.

Sasa ili kukuza huo uchumi kwanini serikali hazifanyi/haifanyi internet kuwa huduma ya bure?

Maana internet tunayotumia inatokana na mkongo wa Taifa ambao umejengwa na Serikali.

Mnaonaje internet ikawa bure?
Labda CCM wawe wammekufa
 
Inawezekana..
Hatujapata Viongozi serious..

Free with fi inatakiwa kila mji..

Na serikali irushe satellite yake ..

Rwanda Wana satellite 9..
Sisi hata moja Tu ya kwetu inatushinda..
Rwanda wanauthubutu sana.
 
Kumbe nchi nyingi wanafanya hizi mambo. Na sisi tunaweza weka kwenye miji mikubwa. Labda kuanza majiji, CBD zetu zote ziwe na free internet. Na kuwe na hotspot sehemu mbalimbali za jiji au jiji zima. Hii ishu hata halmashauri za majiji nafikiri zinaweza fanya. Mbona vyuoni kuna free wifi?
 
Hii internet ya mkongo si miundombinu ni ya serikali. Ifanye kama ilivyo barabara serikali inagharamia lakini zinarahisisha shughuli za uchumi. Tungekuwa na interent ya bure, serikali ingeweza kupata pesa nyingi kuliko ilizowekeza. Tungekuwa na netflix yetu na serikali ingepiga kodi humo, kwa ujumla kungekuwa na streaming services nyingi sana ambazo serikali ingepiga pesa kupitia kodi. Hapo bado biashara na huduma za mitandaoni, elimu ya online, afya, vyuo nk. Mwalimu anafundisha online, daktari anafanya consultation online, mwanasheria anaonana na mteja online nk.
Internet ya bure inaweza fungua mambo na ubunifu wa kushangaza sana kwenye uchumi.
Mkuu mkongo wa taifa unaenda kuungwa kwenye fibre optic inayopita baharini kuunga mabara mfano SeaCom, na hao wanalipwa ndiyo wenye hizo cable zinazopita baharini na kutandaza hizo cable baharini ni gharama sana, pia kuzimaintain likitokea tatizo ni gharama kweli. Hivyo internet ni tofauti kabisa na barabara, mkonga wa taifa unaunganishwa kwenye cable zinazopita baharini na zinamilikiwa na makampuni binafsi ya ulaya na marekani.
Nadhani wahamasishe uwepo wa wireless internet kama nchi nyingine maana uwa ni cheap hivyo watu wanaeza kustream kirahisi maana mabundle yanalipiwa kwa mwezi
 
Kumbe nchi nyingi wanafanya hizi mambo. Na sisi tunaweza weka kwenye miji mikubwa. Labda kuanza majiji, CBD zetu zote ziwe na free internet. Na kuwe na hotspot sehemu mbalimbali za jiji au jiji zima. Hii ishu hata halmashauri za majiji nafikiri zinaweza fanya. Mbona vyuoni kuna free wifi?

Inawezekana sana...
Elon musk ana mpango wa internet bure dunia nzima..
Anataka kurusha satellite yake maalum kwa hilo
 
Clearly hauelewi vizuri internet ni nini. Mkongo wa taifa na ka kipande kadogo sana kwenye hiyo global network. Sehemu kubwa ya miundombinu ya internet inamilikiwa na makampuni binafsi, ni lazima ulipie ukitaka kupitisha data zako.
 
Back
Top Bottom