Kwanini iwekupatwa kwa Jua na siyo kupatwa kwa Dunia?

Kwanini iwekupatwa kwa Jua na siyo kupatwa kwa Dunia?

Za kwenu wana JF?
Naona kunaupotoshi, kama siyo kulisingizia Jua limepatwa kumbe iliyopatwa ni Dunia.

Jua ni Nyota ambayo imezungukwa na sayari takribani kumi na kitu.
Mwezi huzunguka Dunia.

Kupatwa kwa mwezi hutokea pale Dunia inapokuwa katikati ya Mwezi na jua hivyo mwezi hushindwa kuakisi miale ya jua barabara kwa sababu ya na Dunia.

Nakupatwa kwa Dunia ambako ndio mnalisingizia jua ndo limepatwa hutokea pale mwezi unapo pita katikati ya Jua na Dunia, hivyo Dunia hushindwa kupata miale ya mwanga kutoka kwenye Jua. Je, inakuwaje kitendo hiki kiitwe kupatwa kwa Jua na siyo kupatwa kwa Dunia?

Hali yakuwa wakati jua likiendelea kuwaka kama kawaida Dunia ndiyo inayo kuwa imekingwa na Mwezi.

View attachment 391912View attachment 391913View attachment 391914

Dunia inakizunguka jua na mwezi unaizunguka Dunia.
Jua limetulia tuliii linapatwa he sasa hapo?

Ieleweke kuwa kilicho patwa Leo ni Dunia na siyo Jua.
Iendelee kueleweka hivyo, sawa?

View attachment 391911
Hongera kwa kufikiri but you need a little bit to refine your thinking...kupatwa hapa ina maana kuwa kile chanzo tulichokizoea kutupatia mwanga kimezuiwa/kingwa na kitu kingine kutupatia mwanga in this regard.
 
Hapo bado tuna hali ya kuhoji bado ..! Ndio tumekubaliana kua
KUPATWA KWA JUA > yaani miale yake kuzuiliwa na mwezi ili isifike duniani vizuri

KUPATWA KWA MWEZI. ...???????

Hapo kwenye mwezi bado kuna shida

So nitakubaliana na mtoa mada
 
KUPATWA KWA JUA > yaani miale yake kuzuiliwa na mwezi ili isifike duniani vizuri

KUPATWA KWA MWEZI. ...???????
KUPATWA KWA MWEZI > yaani miale ya jua inazuiliwa na dunia ili isifike mwezini.
 
KUPATWA KWA MWEZI > yaani miale ya jua inazuiliwa na dunia ili isifike mwezini.
Kwenye kupatwa kwa jua si tulisema miale ya jua inazuiwa na mwezi isifike dunian

Kwa nini kwenye mwezi isiwe miale ya mwezi inazuiwa na dunia isifike juani ???
Nadhani hapa ndo kuna dought yangu na ya mtoa mada
 
Kupatwa kwa mwezi ni kwamba dunia inakuwa katikati, hivyo mwanga wa Jua hauufiki kwenye mwezi, ila kivuli cha dunia huonekana kwenye full moon. Hii huufanya mwezi kushindwa kung'aa kwa kuwa umezibwa na kivuli cha dunia. Ndo maana tunasema umepatwa.... Obscured....umefichwa..... Eclipsed
 
Hapo bado tuna hali ya kuhoji bado ..! Ndio tumekubaliana kua
KUPATWA KWA JUA > yaani miale yake kuzuiliwa na mwezi ili isifike duniani vizuri

KUPATWA KWA MWEZI. ...???????

Hapo kwenye mwezi bado kuna shida

So nitakubaliana na mtoa mada

Neno eclipse ni neno la kingereza, hebu angalia dictionary. Ili upate eclipse unahitaji vitu vitatu 1) source of light to be obscured/kuzibwa 2) Kitu cha kuziba hiyo light 3) observers. Dunia muda wote inakuwa observer, sisi ndo tunaona kuwa Jua limezibwa (aliyeko juani hawezi ona hiyo phenomenon). Likewise moon eclipse, mwanga uliotakiwa kuja duniani kutoka mwezini unakuwa haupo kwa sababu kivuli cha dunia kinafunika mwezi (hapa mwezi unachukuliwa kama source of light), kivuli cha dunia ni obscure na dunia ni observer. Again ni sisi wa duniani ndo tunaona kuwa mwezi umezimika/umefifia

Kwa hiyo dunia haiwezi kupatwa, ila inashuhudia kupatwa. The same applies kwa sayari zingine na moons zake. Huko Saturn eclipse ni mara kwa mara maana moons zipo nyingi
 
Hongera kwa kufikiri but you need a little bit to refine your thinking...kupatwa hapa ina maana kuwa kile chanzo tulichokizoea kutupatia mwanga kimezuiwa/kingwa na kitu kingine kutupatia mwanga in this regard.
Kilicho zoea kutupatia mwanga kimezuiwa,kwahiyo sisi hatujapata mwanga wake,yaani tumelala Giza,chenyewe kina endelea kutoa mwanga ilasisi tunataabika kwasababu kunakabwana mdogo mwezi kame tuzuia.
Kwahiyo sisi tumepatwa na pigo/tumepatikana/tumepatwa na janga Fulani.
 
mbona unakuwa mgumu kuelewa?...kumbuka kupatwa hapa inamaanisha kuwa mwanga wa chanzo jua au mwezi haufiki duniani this is the only logic here.....so kama tujuavyo mwezi hauzalishi mwanga bali huakisi mwanga wa jua na kuuelekeza duniani kwa hiyo huo mwanga unaotarajiwa kuakisiwa na mwezi na kuelekezwa duniani ukizuiliwa kufika mwezini kisha urudishwe duniani then tunasema mwezi umepatwa na pale mwanga wa jua unapozuiliwa usifike duniani tunasema ni kupatwa kwa jua.
 
Back
Top Bottom