Kwanini James Ward Prowse nahodha wa Southampton haimbwi sana kwenye mipira iliyokufa?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Nimetokea kumkubali sana huyu mwamba nahodha wa Southampton Fc ya kusini mwa Uingereza. Kwanza jinsi anavyojikunja wakati anapiga mipira iliyokufa ni 🔥🔥

Anaitwa James Ward-Prowse yaani fundi kamili sana linapokuja swala la mipira iliyokufa. Amehusika kwenye magoli mengi sana yanayotokana na mipira iliyokufa kuliko mchezaji wowote kwasasa katika EPL.

Ila mwamba haimbwi pengine kwakuwa anachezea klabu ndogo, maana kila siku wanaotukuzwa ni akina Bruno na De Bruyne lakini kwa takwimu hawamkuti huyu mwamba wa Soton katika mipira iliyokufa.

23BBE0AA-915B-4452-BEEC-31D88623442E.jpeg

59CF22C3-AFF5-497A-9EE5-79AF6303ECF3.jpeg
 
Kwani de bruyne na bruno Fernandez wanaimbwa kwa upigaji wa freekick!?

James kwa wachezaji wa sasa hana mpinzani katika hilo, hata pep kasema, sijui wewe unataka aimbwaje hali ulimwengu mzima unatambua hilo, unataka aimbwe kama david Beckham, haliwezekani.
 
Ku

sijasema atukuzwe kama Beckham ila ukiwa unafatilia mijadala utaona kwenye freekick wanapenda sana kuwalinganisha hao jamaa wawili wa jijini manchester
 
Analinganishwa na beckham sababu anajaribu kupitia njia za beckham, kuna vitu beckham aliwafanyia waingireza ndio maana wakamuimba saana freekick dhidi ya ugiriki kama sikosei, kingine jamaa alikuwa na damu ya ustaa.

Katika wapiga freekick bora baada ya juninho mwenye goli kama 77 hivi kuna pele mwenye goli 70 kama sikosei, beckham yupo na goli kama 65 hivi sikumbuki vizuri, sasa huyu ward prowse hata goli 25 za freekick sidhani kama kafikisha, so bado kidogo kupata hiyo heshima.
 
Nimetokea kumkubali sana huyu mwamba nahodha wa Southampton Fc ya kusini mwa Uingereza. Kwanza jinsi anavyojikunja wakati anapiga mipira iliyokufa ni [emoji91][emoji91]

Anaitwa James Ward-Prowse yaani fundi kamili sana linapokuja swala la mipira iliyokufa. Amehusika kwenye magoli mengi sana yanayotokana na mipira iliyokufa kuliko mchezaji wowote kwasasa katika EPL.

Ila mwamba haimbwi pengine kwakuwa anachezea klabu ndogo, maana kila siku wanaotukuzwa ni akina Bruno na De Bruyne lakini kwa takwimu hawamkuti huyu mwamba wa Soton katika mipira iliyokufa.

View attachment 2205110

View attachment 2205111
Huo ni mwamba
 
Back
Top Bottom