Kwanini jezi za Simba zizinduliwe Superdome Masaki, 'sisi' wa Msimbazi sio muhimu?

Kwanini jezi za Simba zizinduliwe Superdome Masaki, 'sisi' wa Msimbazi sio muhimu?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Wenye fedha ndio muhimu msimu huu hapa Simba. Uzinduzi wa jezi za Simba umewalenga wao tu sisi wa Tandale tusubiri masazo baada ya vibopa kuzivaa kwanza.

Hii imetudhalilisha vibaya sana sisi tunaopaka rangi nyekundu usoni viwanjani wakati wa mechi. Naomba matajiri waende kuishangilia timu.

Wakati matajiri wanapelekewa jezi Masaki na sisi makabwele tuambiwe wapi tukapange foleni ya kununua jezi wakati huohuo. Yaani tofauti iwe moja tu ya matajiri wenye sh. 250000 wanapelekewa wakati wanakula na kunywa na sisi wenye eflu 45000 tunakwenda kukanyagana kupata jezi hapo zinapouzwa ili kila mtu awe na haki sawa ya kuwa wa kwanza kuvaa jezi mitaani.
 
Wenye fedha ndio muhimu msimu huu hapa Simba. Uzinduzi wa jezi za Simba umewalenga wao tu sisi wa Tandale tusubiri masazo baada ya vibopa kuzivaa kwanza.

Hii imetudhalilisha vibaya sana sisi tunaopaka rangi nyekundu usoni viwanjani wakati wa mechi. Naomba matajiri waende kuishangilia timu.
UZINDUZI haufanyiki ndani ya nyumba ya mtu hata wewe unaweza ukafika Masaki siku husika.
 
Hivi karibuni umeona wapi tukio lolote la Simba likifanyika pale msimbazi!?
Kifupi msimbazi pale kwa Sasa pote pamepangishwa na Simba inaingiza mablioni ya fedha ambayo yanaisaidia Kilabu (sijui yanasaidiaje ila yanasaidia)
 
Wakati wenye fedha wanapelekewa jezi superdome wakati wameketi wakila na kunywa kwanini sisi makapuku na sisi tusiambiwe wapi tukazipate siku na muda huohuo?. Hii maana yake wenye fedha wawe wa kwanza kuzivaa ndipo tufuate sisi makabwela, hapo veepe!!! Jamani wenzangu tutafuteni hela ili kuepuka dharau kama hizi.

Kwani ukumbi ule wa superdome masaki unatosha watu wangapi wenye laki 2.5?
 
Tafuta Pesa mdogo wangu
Laki 2.5 sina lakini elfu 45 za jezi na elfu 5 ya kuingia uwanjani ninzazo. Kwahiyo sisi wenye hela hii hatuna thamani? Hatustahili kuwa wa kwanza kuvaa jezi ya Simba.
 
Jezi classic kama Ile huwezi izindulia manzese
Issue sio kuzindua bali kudharauliwa. Kwamba hatuwezi kuzivaa kabla ya matajiri kuzivaa kwanza. Basi wavae wenyewe tu. Dharau ya hali ya juu hii, tutaweka wapi nyuso zetu.. Wakati matajiri wanapatiwa huo masaki wakati huohuo na sisi tuambiwe tukapange foleni wapi tupata jezi. matajiri wanavaa na sisi makabwela tunavaa japo kwa kukanyagana.
 
Moja ya nyuzi za hovyo kuwahi kuandikwa katika historia ya internet.
Nimeziona jezi kwenye video pale superdome, ni jezi za hovyo sana, ile shingo ni kama shumizi ya mama anaenyonyesha. Yaani anaweza kupitisha nyonyo pale shingoni mtoto anyonye, panavutikna vizuri kabisa. Kitambaa ni kama vile vya kufunika dashboard isipate mavumbi au yenye hitilafu.
 
Back
Top Bottom