UZINDUZI haufanyiki ndani ya nyumba ya mtu hata wewe unaweza ukafika Masaki siku husika.Wenye fedha ndio muhimu msimu huu hapa Simba. Uzinduzi wa jezi za Simba umewalenga wao tu sisi wa Tandale tusubiri masazo baada ya vibopa kuzivaa kwanza.
Hii imetudhalilisha vibaya sana sisi tunaopaka rangi nyekundu usoni viwanjani wakati wa mechi. Naomba matajiri waende kuishangilia timu.
😂😂😂😁😁😁Unafikir ni vijora vile mpaka vikazinduliwe kariakoo????
Wakati wenye fedha wanapelekewa jezi superdome wakati wameketi wakila na kunywa kwanini sisi makapuku na sisi tusiambiwe wapi tukazipate siku na muda huohuo?. Hii maana yake wenye fedha wawe wa kwanza kuzivaa ndipo tufuate sisi makabwela, hapo veepe!!! Jamani wenzangu tutafuteni hela ili kuepuka dharau kama hizi.Hivi karibuni umeona wapi tukio lolote la Simba likifanyika pale msimbazi!?
Kifupi msimbazi pale kwa Sasa pote pamepangishwa na Simba inaingiza mablioni ya fedha ambayo yanaisaidia Kilabu (sijui yanasaidiaje ila yanasaidia)
Tafuta Pesa mdogo wangusina laki 2.5
Issue sio kuzindua bali kudharauliwa. Kwamba hatuwezi kuzivaa kabla ya matajiri kuzivaa kwanza. Basi wavae wenyewe tu. Dharau ya hali ya juu hii, tutaweka wapi nyuso zetu.. Wakati matajiri wanapatiwa huo masaki wakati huohuo na sisi tuambiwe tukapange foleni wapi tupata jezi. matajiri wanavaa na sisi makabwela tunavaa japo kwa kukanyagana.Jezi classic kama Ile huwezi izindulia manzese
Nimeziona jezi kwenye video pale superdome, ni jezi za hovyo sana, ile shingo ni kama shumizi ya mama anaenyonyesha. Yaani anaweza kupitisha nyonyo pale shingoni mtoto anyonye, panavutikna vizuri kabisa. Kitambaa ni kama vile vya kufunika dashboard isipate mavumbi au yenye hitilafu.Moja ya nyuzi za hovyo kuwahi kuandikwa katika historia ya internet.