Kwanini Jf imejaa member waoga ?

Mkuu hebu fanya utafiti wako kisawa sawa utajua ukweli wa akaunti za majina feki huko fesibuku na tuita ,

japo wapo pia wanaotumia majina ya kweli alkadhalika hata fj pia sio wote wanatumia majina feki bali majina yao halisi,

Usiniombe mifano tafadhali ,
 
lakini unapokuja ndani ya himaya ya maGREAT THINKER wengi wao ni waoga hata kuweka majina yao au picha zao au hata kueleza walikosoma,wanakoishi au hata wanakopendelea kutembelea.
Una milioni saba za kumlipia kila mwana JF tubadilishe majina fasta?
 
Si uoga bali ni utashi wa mtu mwenyewe .. Hata huko fb ni asilimia ndogo sana wanatumia majina yao halisi japo walipojiunga walikuwa wanatumia majina kamili ..
 
Kwa hiyo hatujiamini kama tupo sahihi katika yale tunayoamini ?
 
Si uoga bali ni utashi wa mtu mwenyewe .. Hata huko fb ni asilimia ndogo sana wanatumia majina yao halisi japo walipojiunga walikuwa wanatumia majina kamili ..
lakini angalau watu hawana woga,tofauti na great thinker wa hapa.
 
Mtu hajamsoma Publius wala Tocqueville, unaanzaje kumuelimisha kuhusu umuhimu wa anonymity katika online forums?
 
Ile bili ya kule Naiii umeisikia lkn?
 
Unatumia nguvu nyingi na janja nyingi za nini kuwataka watu wajidisclose humu ndugu ili iweje??!! Wengine interest zao humu ni kujifunza vitu mbalimbali vya maisha na kuwafunza wengine pia vitu wanavyojua sio kutafuta umaarufu wa kujulikana. Kama interest yako wewe ni kujulikana ili upate faida fulani sera ya JF inakuruhusu kama inavyowaruhusu wengine pia kulinda ID zao. Na kama hii inakukera, FACEBOOK inakufaa zaidi.
 
Unaelewa maana ya uoga? Kuonyesha sura ndio kigezo cha ujasiri? Wanaoficha uhalisia wao humu unafiri hawajuani? Je umekosa mbinu za kuwafahamu watu humu? Wewe unajipambambanua huogopi nini?
 
Hebu rudi na ukachukue kamusi ya IT ili upate kujua nini maana ya 'web forum' na washiriki hujiunga vipi na hutumia majina yapi...

La hasha tembelea web forums mbalimbali na uone watumiaji wake hutumia majina gani...

Zaidi tembelea hapa upate kuelimika juu ya uga wa 'web forums':
Internet forum - Wikipedia
 
Kwan jaman lazima tujuane kwa majina halisi mbona hivi kwa anonymity inatosha sana,,au ni campaign ya sizonje kutudaka maana naona nyuzi za kutambuana zimezidi tumechoka em mtupumzishe
 
Kwa sababu za kumili fake ID, imepelekea mazingira ya JF kuwa salama na yenye uhuru kuliko social media zozote...


Humu tunaweza kuongea chochote liwe baya au zuri, jema au la karaha...

Hizo sehemu nyingine watu wana post mazuri yao tu...

Ushawahi ona member wa JF kakamatwa sababu ya kupost chochote, ila hiyo mitandao mengine watu wanakamatwa ovyo kwa sababu ya ujinga...


Cc: mahondaw
 
Tukisema tufate wazo lako wengi atutaonekana...adi huyo aliekutuma uwezi kumuona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…