Kwanini Jumaa Aweso anaonekana kukubalika zaidi?

Kwanini Jumaa Aweso anaonekana kukubalika zaidi?

Wizara ya maji haina ugumu wowote kama kuna bajeti, ukishakua na bajeti kinachobaki ni usimamizi tu ambao mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufanya.

Hakuna mambo yoyote ya ajabu kutoka kwenye wizara ya maji ambayo yashafanyika tangu yeye awe Waziri. Tungemuona wa maana sana kama angegusa kwenye eneo la umwagiliaji ambalo kwa kiasi kikubwa limesahaulika sana.

Inawezekana pengine Awesso akawa ni kiongozi bora lakini hii wizara aliyopo haiwezi kuwa mizani nzuri ya kupima ubora wake.

Zingine zilizobaki ni ngojera tu
Umwagiliaji iko kilimo labda wasiliana na Bashe
 
Kwanini Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anaonekana ni moja ya Mawaziri wanaoongelewa vizuri zaidi ana nini hasa cha ziada tofauti na wenzake?

Itakumbukwa kuwa Aweso ni moja ya mawaziri wapya ambaye alianza majukumu ya Naibu Waziri wa Maji mwaka 2017 na baadaye kuja kuwa Waziri kamili wa Maji.

Huku wengine wakiwa ni wazoefu kwenye uwaziri shida ni nini
Keshazijua Passwords za Mama Kurembua.
 
Sidhani kama uko sahihi unayo rekodi ya hali ya upatikanaji maji vijijini ulivyo kwa sasa kupitia miradi ya RUWASA ukilinganisha na miaka ya nyuma unless kama una tatizo binafsi na aweso

Awesome umeanza kujisifia. Unautaka urais.
 
Mimi nadhani kinachombeba Aweso ni kwa sababu ni Mtoto wa Mama Ntilie na hakutokana na mfumo wa kutumia jina la Baba au Babu kwenye uongozi ndio maana anajitahidi kutekeleza majukumu yake vizuri ndio maana hata bungeni huoni akizozana na wabunge

Aweso hakubaliki popote basi tu. Pamoja na Makamba kuboronga lakini ana state appeal kuliko Aweso.
 
Kwanini Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anaonekana ni moja ya Mawaziri wanaoongelewa vizuri zaidi ana nini hasa cha ziada tofauti na wenzake?

Itakumbukwa kuwa Aweso ni moja ya mawaziri wapya ambaye alianza majukumu ya Naibu Waziri wa Maji mwaka 2017 na baadaye kuja kuwa Waziri kamili wa Maji.

Huku wengine wakiwa ni wazoefu kwenye uwaziri shida ni nini

Aweso umeanza kujipigia kampeni. Tatizo unafanya kazi kwa kujitangaza ili ugombee urais. Ridhika na cheo ulichonacho urais uwe ni majaliwa ya mola.
 
Kwanini Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anaonekana ni moja ya Mawaziri wanaoongelewa vizuri zaidi ana nini hasa cha ziada tofauti na wenzake?

Itakumbukwa kuwa Aweso ni moja ya mawaziri wapya ambaye alianza majukumu ya Naibu Waziri wa Maji mwaka 2017 na baadaye kuja kuwa Waziri kamili wa Maji.

Huku wengine wakiwa ni wazoefu kwenye uwaziri shida ni nini
Anafanya kazi zinaonekana
 
Back
Top Bottom