Maadui wakubwa wa taifa hili wamekuwa siku zote ni ujinga, maradhi na umasikini.
Miaka 60 ya uhuru leo tungali humo humo.
Hali halisi tishio jipya la corona
Leo hii pamoja na tahadhari zote za wataalamu wabobezi, ujinga ungali umetughubika vilivyo.
Kwa maana halisi, ujinga ni kudhani wajua kumbe hujui, ni kutokuelewa, au kutokufahamu. Ujinga si tusi. Elimu huondoa ujinga.
Tulipo leo bado tuna wanaodhani wataalamu ndiyo wajinga na kuwa eti kutokea vijiweni wao ndiyo werevu. Hiyo ni shughuli pevu.
Leo hii tunakabiliwa na gonjwa la hatari zaidi linaloua ghafla ghafla, ndani ya mengine mengi ambayo nayo bado ni kizungumkuti.
Umasikini wetu nao uko pale pale. Zaidi sana hata wabunge wetu nao ndiyo wanazidi kulia njaa. Huku mitaani na vijijini kutakuwa je?
Tunaponea wapi kama taifa bila ya kuwa na mkakati sahihi kutokea juu?
Hii bila ya suluhu kutokea kwake Mama Samia, zikiwamo busara zake, tusipoangalia tutaangamia wengi.