Uchaguzi 2020 Kwanini kampeni za mwaka huu zimepooza sana?

Uko sahihi kabisa mkuu hasa hizo sababu mbili za mwisho (6 & 7). 👊👊👊
 
Rushwa imekosekana, pili chama tawala siyo tena kila cha 2015 wakati kilipokuwa ICU (mahututi Hospital ya Apollo India) na Zito na Lipumba kuvuruga upinzani!! Leo hii hakuna cha ACT-Wazalendo, Chadema, TLP, UDP, NCCR, NRA, TADEA,CCK wala mamake CUF! wote hao hawapati mbunge hata mmoja Bara ila CHADEMA wanaweza kupata angaa 10!!!!! Kosa la upinzani walilolifanya na kutenda 2015 litawagarimu mmno mno mno kwa generation(vizazi) vinne vijavyo!
 
Ukweli ni kwamba wapinzani wamebanwa sana uchaguzi huu ulikuwa ni wakuususia tu basi wagombea wameamua kupambana katk hayo hay mazingira magumu
 
Toka kuzinduliwa kwa kampeni yaan sehemu nyingi za dar Utadhani Hakuna uchaguzi mwaka huu... Story za simba na yanga ndio zimetapaa... SIJASIKIA POPOTE WATU WAKIJADILI CCM AU CHADEMA ETC..
 
Toka kuzinduliwa kwa kampeni yaan sehemu nyingi za dar Utadhani Hakuna uchaguzi mwaka huu... Story za simba na yanga ndio zimetapaa... SIJASIKIA POPOTE WATU WAKIJADILI CCM AU CHADEMA ETC..
Hata hiyo hamasa iliyojitokeza kwa muda wa wiki mbili tatu hivi ni kwa sababu ya ujio wa Tundu Lissu, bila hivyo mwaka huu ingekua baridi zaidi. Hata hivyo ubaridi wa ghafla tena umesababishwa na mwenendo wa mchakato katika kuwapitisha wagombea baada ya NEC kuendekeza enguaengua ya wagombea, wananchi wameamua kuendelea na yao kwa sababu hata hao wanaowachagua hakuna la maana wanaenda kufanya huko Bungeni. Ni bora ligi kuu ya VPL ianze na hiyo ya EPL ambazo waTanzania wanapata furaha kuliko kupoteza muda kwenye kampeni, refer SIMBA DAY na YANGA DAY. Watanzania wanapenda furaha lakini wananyimwa na NEC.
 
Wapinzani wanafanya siasa katika mazingira magumu sana,
1. Mazingira ya kufungiwa kwa miaka mitano mfululizo.
2. Mazingira ya kufunguliwa kufanya siasa na kupangiwa cha kuongea.
3.Mazingira ya kukosa fedha za kutosha kufacilitate movements za kampeni, Wapinzani hawana ruzuku ya kutosha kufanya kampeni kugusa miji na vijiji vyote, CCM yenyewe pamoja na ruzuku yao kubwa bado huwa haitoshi ndio maana kuna marafiki wachangia kampeni, nawashangaa wanaowanga wana CDM kwa kuomba michango.
4. Upinzani kunyimwa positive publicity katika vyombo vya habari.
5. Waunga mkono juhudi wamepunguza imani na hamasa kwa wapiga kura.
6. Siasa kuwa zakusaka vyeo na si kuwatetea wanachi.

Mambo ni mengi, ni kama vile wanachi wamesusa. Wamewaachia wasakavyeo wapambane na hali zao.
 
Watu wamemkataa Tundu Lissu
mkuu kumbe upo si ulisema lissu anakatwa sasa mkuu njoo na lingine kwamba lissu haendi ikulu, maana maneno yako yanambariki sana lissu , na kama vipi nikuombe mkuu kachukue kadi ya chadema mkuu , nikutakie utekerezaji mwema mwana mageuzi ya kweli
 
Ni simpo
1.Vyombo vya habari vimebanwa kutangaza sera za vyama.Hiki kilikuwa ni kipindi cha kuongeza mauzo ya magazeti na kuongeza wasikilizaji na waangaliaju wa TV ila imekuwa tofauti.

2.Midahalo ya wagombea hakuna

3.Upendeleo wa wazi wazi wa NEK

4.Wagombea wakinana mama kunyimwa fomu na kukatwa kionevu.

5.Wachambuzi wa siasa hawapo tena.

6.Dhulumq za NEC huko zanzibar.

Natabiri wapiga kura wengi hawatajitokeza kupiga kura.
 
Nasikia ata vyama kujitafutia misaada ya fedha za uchaguzi nayo imepigwa pini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…