Wapinzani wanafanya siasa katika mazingira magumu sana,
1. Mazingira ya kufungiwa kwa miaka mitano mfululizo.
2. Mazingira ya kufunguliwa kufanya siasa na kupangiwa cha kuongea.
3.Mazingira ya kukosa fedha za kutosha kufacilitate movements za kampeni, Wapinzani hawana ruzuku ya kutosha kufanya kampeni kugusa miji na vijiji vyote, CCM yenyewe pamoja na ruzuku yao kubwa bado huwa haitoshi ndio maana kuna marafiki wachangia kampeni, nawashangaa wanaowanga wana CDM kwa kuomba michango.
4. Upinzani kunyimwa positive publicity katika vyombo vya habari.
5. Waunga mkono juhudi wamepunguza imani na hamasa kwa wapiga kura.
6. Siasa kuwa zakusaka vyeo na si kuwatetea wanachi.
Mambo ni mengi, ni kama vile wanachi wamesusa. Wamewaachia wasakavyeo wapambane na hali zao.