Pamoja na kufunguliwa kwa dirisha la kampeni, lakini dalili zote zinaonyesha Wananchi hawana hamu na kampeni, wanaofuatilia kampeni ni wachache ukilinganisha na mwaka 2015.
Nimejaribu kuangalia ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai. CHADEMA wao wanategemea watu wasio na kazi maalumu na ndiyo kinachowafanya waanze kampeni muda wa saa 11 ambapo watu wanatoka sehemu za kazi.
CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni? Anyway, mwaka huu watu wengi wanafatilia siasa wakiwa wanapambana na maisha yao.
NB: WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE ILA HAWADHANI KAMA ITAWEZEKANA
"dalili zote zinaonyesha Wananchi hawana hamu na kampeni".
Kwa maoni yangu nadhani si kwamba watu hawana hamu na kampeni, bali inawezekana ni kwa sababu 2.
(1) Kutokana na awamu hii ilivyokuwa watu wamesha kata tamaa na ccm, pengine wanaona hata wakifuatilia kampeni za ccm hakuna jipya kuhusu maisha yao, hasa kwa namna ccm inavyo lazimisha ushindi. Wanajua nini kitaendelea ccm itakapo jiweka madarakani baada ya uchafuzi.
(2) Kutokana na awamu hii ilivyokua pengine watu bado wana hofu na maisha yao kuhudhuria mikutano ya upande wa upinzani. Kwa sababu wanajua kwa upande huo polisi hawakawii kukinukisha.
Kwa kuwa kampeni ndio zimeanza, pengine wengi bado hawajaamini kwamba ni kweli imeruhusiwa kukusanyika ama ni mtego ili watu tuumizane? Si unajua tena kila mtu ana uelewa wake.
"ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai".
Ukiondoa walio na vyeo ndani ya chama/serikalini walio baki wote walishavunjwa viuno sio hai tena. Kwa mfano idadi ya walio jitokeza kuomba uteuzi kwenye nafasi za ubunge haija wahi kutokea katika historia ya nchi hii. Kipropaganda wanakwambia ni kwa sababu ya utendaji kazi wa awamu ya 5. Lakini ukweli ulio jificha ni kwamba watu wamejifunza katika muhula wa kwanza wa JPM. Na kama akiingia muhula wa pili basi hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa sababu anamaliza muda wake na hana cha kupoteza. Kazi ambayo haina longolongo na ni ya uhakika nikuingia mjengoni. Ukiondoa mshahara, posho ya kila kikao bora tu uwe umesaini kwamba upo bila kujali kwamba utachangia, utashangiria ama utalala tu kwenye kiti chako lakini lazima 340,000 itakuhusu. Bado kuna kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 200 kina kusubiri ndani ya miaka mitano. Kwa nini watu wasijitokeze kwa wingi. Na pia uhai wa ccm unao onekana sio uhalisia. Kuna makundi mawili, kundi la masikini ambao kwa sasa tunaitwa wanyonge, kundi hili inapofika wakati wa kampeni kwao inakuwa ni kama sikukuu wanapata shati, flana, magauni, madera, kanga na vitenge vipya kwa sare ya chama na wanakuwa wamepata mahali pa kwenda ili siku iishe kwa shangwe. Na kundi jingine ni la wapenzi/mashabiki wa wasanii, hawa nao wanafuata shangwe na ndio hapo watu tunapo dhani kuwa ccm inajaza watu kwa maana yakupendwa/kukubalika.
"CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni?"
Hawana akiba yoyote kiongozi,miaka zaidi ya 50 madarakani na hasa yaliyo fanywa na awamu hii kama yatawekwa kinamna ya hoja ili yajadiliwe basi itakuwa ngumu kwa ccm kuyatetea kwa hoja.
"WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE".
Lissu kushinda sio muujiza na hata ccm wenyewe wanajua hilo, ndio maana unaona kuna sarakasi nyingi. Ki ukweli JPM hayuko vizuri katika ujengaji hoja ukimpambanisha na Lissu.
Na suala la Lissu kushinda ama kushindwa rudia kutafakari kauli za aina tatu na uangalie mambo yanavyo kwenda halafu utajua muujiza utakuwa upi? Tafakari kauli hizi:
"Nikuteue mimi, nikupe gari na mshahara nikulipe mimi halafu umtangaze mpinzani?"-JPM
"Chama kilichopo madarakani ndio kinacho nufaika na dola kubaki madarakani, kanu iliondoka madarakani kwa sababu ilishindwa kuitumia dola kubaki madarakani". - Dr Bashiru
"Uchaguzi ukiwa huru na wa haki, ccm ijiandae kukabidhi ikulu". - Polepole
Kutokana na kauli hizo ambazo hata mimi ambae si msomi lakini nimezielewa. Muujiza hapa sio Lissu kushinda, bali muujiza ni tume ya uchaguzi (tawi la ccm) kumtangaza Lissu kwamba ameshinda.