Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Magu alifungia siasa kwa miaka mitano, akawasomesha namba wananchi.Pamoja na kufunguliwa kwa dirisha la kampeni, lakini dalili zote zinaonyesha Wananchi hawana hamu na kampeni, wanaofuatilia kampeni ni wachache ukilinganisha na mwaka 2015.
Nimejaribu kuangalia ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai. CHADEMA wao wanategemea watu wasio na kazi maalumu na ndiyo kinachowafanya waanze kampeni muda wa saa 11 ambapo watu wanatoka sehemu za kazi.
CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni? Anyway, mwaka huu watu wengi wanafatilia siasa wakiwa wanapambana na maisha yao.
NB: WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE ILA HAWADHANI KAMA ITAWEZEKANA
Akafungia bunge, wananchi wakanyimwa ushiriki wao kwa shughuli za serikali.
Wakazuia taasisi za kiraia ambazo hutoa elimu ya uraia na ushiriki wa wananchi kwenye shughuli za umma.
Akaziminya halmashauri zote zikamtegemea yeye kaamkaje hivyo wananchi wakawa hawana sauti tena hata huko serikali za mitaa.
Serikali yake ikafumbia macho utekaji, watu kupigwa risasi, vijana waliokuwa wakishiriki siasa wakatekwa, wakafunguliwa makesi.
Wanasiasa wakafunguliwa makesi, wakapigwa na mapolisi, wakafungwa na wakafilisiwa.
Vyombo vya habari vikazuiwa kutangaza habari za siasa tena wala masuala ya kijamii radio zikaamua kupiga bongo flava na singeli kwa miaka mitano wananchi wakaamua kuunga mkono bongo flava.
Tume ya uchaguzi kufanya uhuni kuchezea Sanduku la kura na uchaguzi wa serikali za mitaa.
Vyombo vya habari haturuhusiwi tena kutangaza mikutano ya vyama vingine isipokuwa ccm tu wakati haina mvuto tena kwa wananchi.
Akajitia mjuaji akaanza kununua wapinzani uchwara ambao wananchi walipoteza damu zao kuwapigania.
Wananchi wakatishwa kwa matukio ya utekaji na maiti kuokotwa kwenye viroba, na waliopigwa risasi hadharani bila hata aibu.
Nani atakuwa na hamu na uchaguzi tena ??
Magufuli katuharibia nchi sana.