Uchaguzi 2020 Kwanini kampeni za mwaka huu zimepooza sana?

Uchaguzi 2020 Kwanini kampeni za mwaka huu zimepooza sana?

Pamoja na kufunguliwa kwa dirisha la kampeni, lakini dalili zote zinaonyesha Wananchi hawana hamu na kampeni, wanaofuatilia kampeni ni wachache ukilinganisha na mwaka 2015.

Nimejaribu kuangalia ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai. CHADEMA wao wanategemea watu wasio na kazi maalumu na ndiyo kinachowafanya waanze kampeni muda wa saa 11 ambapo watu wanatoka sehemu za kazi.

CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni? Anyway, mwaka huu watu wengi wanafatilia siasa wakiwa wanapambana na maisha yao.

NB: WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE ILA HAWADHANI KAMA ITAWEZEKANA
Magu alifungia siasa kwa miaka mitano, akawasomesha namba wananchi.

Akafungia bunge, wananchi wakanyimwa ushiriki wao kwa shughuli za serikali.

Wakazuia taasisi za kiraia ambazo hutoa elimu ya uraia na ushiriki wa wananchi kwenye shughuli za umma.

Akaziminya halmashauri zote zikamtegemea yeye kaamkaje hivyo wananchi wakawa hawana sauti tena hata huko serikali za mitaa.

Serikali yake ikafumbia macho utekaji, watu kupigwa risasi, vijana waliokuwa wakishiriki siasa wakatekwa, wakafunguliwa makesi.

Wanasiasa wakafunguliwa makesi, wakapigwa na mapolisi, wakafungwa na wakafilisiwa.

Vyombo vya habari vikazuiwa kutangaza habari za siasa tena wala masuala ya kijamii radio zikaamua kupiga bongo flava na singeli kwa miaka mitano wananchi wakaamua kuunga mkono bongo flava.

Tume ya uchaguzi kufanya uhuni kuchezea Sanduku la kura na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Vyombo vya habari haturuhusiwi tena kutangaza mikutano ya vyama vingine isipokuwa ccm tu wakati haina mvuto tena kwa wananchi.

Akajitia mjuaji akaanza kununua wapinzani uchwara ambao wananchi walipoteza damu zao kuwapigania.

Wananchi wakatishwa kwa matukio ya utekaji na maiti kuokotwa kwenye viroba, na waliopigwa risasi hadharani bila hata aibu.


Nani atakuwa na hamu na uchaguzi tena ??
Magufuli katuharibia nchi sana.
 
Zamani kulikuwa na ruhwa kuanzia uteuzi mpaka miwsho.wa kampeni kwa hiyo mambo yalikuwa moto.
Pia kipindi hicho watu walikuwa na pesa zinazokosa kazi kwa hiyo kuwapa wanasiasa haikuwa shida ila sasa mambo ni ngumu kila mtu anajua thamani ya pesa.

Hapo nyuma nakumbuka nilinunua gari yangu ambayo town hii nilikuwa peke yangu,
Sasa ukiingia kwenye gari tu utashangaa mtu anagonga kioo ukishusha tu ana anza kutoa sifa anazungumza kisha anaomba na pesa, unachomoa unampa, ila kwa sasa hata wakija na sifa zao nawaangalia tu,
Mpaka wameamua kuomba hata mia tano sitoi.
Wengi hawataenda kwenye kampeni ila kwenye kupiga kura wataenda na wanamjua mgombea watakaempa ambaye alichokifanya kinaonekana lakini wapo wapinzani watakaobadilika siku ya kupiga kura akiingia tu kwenye chumba anawaza maendeleo hapo moja kwa moja inamjia sura ya magu.
 
mkuu uko sawa ila niseme tu chama dola hasa viongozi wa juu wameisha ona aina ya mchezo ulivyo mgum , japo twaongea kujifuraisha hum tu thats hata hii engua inawafeva kidogo but niseme tu ccm pamoja na viti ambavyo tiyari wanavyo vikiongezeka zaidi katika uchaguzi havitazidi 25 nakwambia , msicheze na uchaguzi mkuu , mfano jiulize kama chama dola kinafikili uchaguzi huu ni mwepesi why wanatumia gharama kubwa , kwa macho ya rohoni huu ni uchaguzi mgum kuwahi tokea tz na hivihivi kimasiara uanweza shangaa chadema inaondoka na taulo ya mtu , msemo wa gwajima
Uhuru wa kujieleza na Ni haki yako kusikilizwa.
 
Ukweli utatuweka huru, uchaguzi huu umeharibiwa na gia ya angani 2015 wapinzani hawaaminiki tena. Hata hizi kelele unazosikia mitandaoni ni vijana ambao hawakupiga kura 2015 sababu ya umri.

Kingine wapinzani hawapo serious Sana kupambana na CCM huwezi kuishinda CCM bila wao kuungana km ilivyokuwa 2015. Hawana malengo, wamejaa viburi na ubinafsi.

CCM sio ile ya 2015 iliyoingia kwenye uchaguzi ikiwa ndembendembe kwa kashfa za rushwa na kutowajibika ipasavyo. Hii ya 2020 inamtaji mkubwa wa wananchi wanaoiunga mkono hasa watu wa hali ya chini. Ikumbukwe ndipo wapigakura wengi walipo.

Lissu na Membe hawana ushawishi wala mvuto kwa wananchi. Inaonekana 'bora zimwi likujualo... Aina za kampeni hasa Lissu inaonekana hakujiandaa kilicho mleta ni hasira za risasi 16. Kauli zake nyingi ni utegemezi kwa mataifa ya nje. Hii imempotezea sana hata ile imani ndogo wananchi walokuwa nayo juu yake.
Huu ni ukweli au hisia tu ?
 
Inasikitisha. Vyombo vya habari vimechukua nafasi kubwa ya kugeuza kampeni na Uchaguzi kuwa na muelekeo wanaotaka. Si wananchi tumekosa picha kamili ya nini kinaendelea!
 
Kiufupi nchi hii tasnia ya habari imeingiwa na matapeli na washamba wa kisiasa
 
Mnapowashangaa waandishi wa habari na vyombo vya habari, shangaeeni na TCRA ambao kila siku wanatunga kanuni ili CHADEMA na upinzani wasisikike. Kwani ni nani anataka kufungiwa bwana?
 
Ukiona mgombea wako au chama chako hakiripotiwi sana na vyombo vya habari fahamu kuwa wanafanya kampeni zilizo kinyume na maadili ya uchaguzi. Matusi, uchochezi, vitisho, uchonganishi ndio vinatawala. Sasa vyombo vya habari haviwezi kuripoti vitu kama hivyo.
 
Mnapowashangaa waandishi wa habari na vyombo vya habari, shangaeeni na TCRA ambao kila siku wanatunga kanuni ili CHADEMA na upinzani wasisikike. Kwani ni nani anataka kufungiwa bwana?
Kwani CHADEMA wanashindwa nini kutimiza masharti ya hizo kanuni? Nini kinawazuia kucomply na hizo kanuni?
 
Ndivyo wanavyotaka.. awamu hii ilianza kutunisha mbawa zake toka bungeni hawakutaka liwe live ili wananchi wasione wawakirishi wao!..

Vyombo vya habari ilitakiwa iwe ni chemchem ya kujibu maswali kwa kuwahoji wahusika juu ya maswala mbalimbali mfano.. kukosekana kwa mikopo vyuoni,maswala ya ajira,kunatakiwa kuwe kuna mjadala juu ya elimu yetu je,inakidhi vipi ktk kutatua uhaba wa ajira..? Hayo ni baadhi ya hoja na maswali yaliyopaswa yajibiwe.. tupo tu tunasikilizishwa watu walewale wanaolalamika nchi ikinyonywa wakati huyohuyo nae amekuwepo serikallini kwa miaka 20! Tena anarudi na kuuhadaa uma!..

Vyombo vya habari vingi vinaonyesha yaliyofanywa tu hata hawaonyeshi ambayo hayajafanywa.. inatakiwa wawe chachu pia ya kuionyesha serikali matatizo,inatakiwa pia iwahoji watu ili serikali ijue watu wake wanataka Nini.. tumechoka kila siku kusema hoyeeeee..
 
Kwani Chadema wanashindwa nini kutimiza masharti ya hizo kanuni? Nini kinawazuia kucomply na hizo kanuni?
Kwendra huko. Hata huelewe unachoandika hapa. Nitapoteza muda kubishana na wewe.
 
Back
Top Bottom