MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Kampuni za kibiashara ni miongoni mwa vyanzo vya mapato kwa mashirika ya hisani (charity organizations) kwenye utekelezaji wa miradi na program mbalimbali. Utafutaji wa fedha kutoka kwenye kampuni hizi, kitaalamu unajulikana kama “Corporate Fundraising” . Kuna njia mbili za uchangiaji unaofanywa na kampuni za kibiashara kwa mashirika ya hisani, njia hizo ni kama ifuatavyo;
- Kampuni kuanzisha Taasisi maalum ambayo itakuwa na lengo la kusaidia mashirika ya hisani. Taasisi hii kiuongozi inakuwa tofauti na uongozi wa kampuni husika. Kitaalamu, Taasisi hizi zinajulikana kwa jina la “Corporate Foundations” . Kwa hapa kwetu Tanzania, mfano wa Taasisi hizi ni; CRDB Foundation chini ya benki ya CRDB, Vodacom Tanzania Foundation, chini ya kampuni ya Vodacom, DP World Foundation, chini ya DP World na nyinginezo.
- Kampuni kuanzisha “program” maalum kwa ajili ya kuchangia mashirika ya hisani. Kitaalamu inaitwa “Corporate Giving Programmme”. Bajeti ya programu hii hutegemea mapato ya kampuni kwa mwaka husika. Kampuni zote kubwa zina programu hizi.
Kwanini kampuni zinachangia mashirika ya hisani?
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaeleza kwanini kampuni zinapaswa kuchangia mashirika ya hisani. Miongoni mwa sababu hizo ni kama ifuatavyo;
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaeleza kwanini kampuni zinapaswa kuchangia mashirika ya hisani. Miongoni mwa sababu hizo ni kama ifuatavyo;
- Corporate Productivity: Sababu hii imejikita kwenye dhana ya kwamba, uchangiaji wa kampuni kwa shirika la hisani unaongeza faida kwa kampuni na kuongeza thamani kwa wanahisa. Kampuni zinazochangia mashirika ya hisani kwa sababu hii, wanafadhili miradi yenye sifa zifuatazo;
- Miradi itakayosaidia kutangaza bidhaa au huduma za kampuni (sponsorships, cause-related marketing)
- Miradi inayoleta morali ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni husika.
- Miradi inayojenga taswira nzuri ya kampuni kwa jamii.
- Miradi ya utafiti ambayo itaipunguzia kampuni gharama kwenye shughuli za utafiti.
- Ethical Altruistic Reason: Sababu hii imejikita kwenye dhana ya kwamba; kimaadili kampuni pamoja uongozi wake unajukumu la kuisadia jamii ili kujenga mahusiano mazuri. Kampuni zinazochangia mashirika ya hisani kwa sababu hii, wanafadhili miradi yenye sifa zifuatazo;
- Miradi ambayo itatatua matatizo ya jamii kama ukosefu wa maji, ukosefu wa shule/upungufu wa madarasa n.k. Mara nyingi miradi hii inapaswa kutekelezwa eneo/maeneo ambayo kampuni ina ofisi au ina wateja wa bidhaa/huduma zake.
- Miradi ambayo itatoa nafasi kwa wafanyakazi wa kampuni husika kushiriki kwenye shughuli za kijamii.
- Political Reason: Sababu hii imejikita kwenye dhana ya kwamba; uchangiaji wa kampuni kwa mashirika ya hisani unaijengea kampuni ushawishi kwa jamii pia unaipa kinga kampuni dhidi ya maamuzi ya serikali ambayo yanaweza kuathiri biashara. Kampuni zinazochangia mashirika ya hisani kwa sababu hii, wanafadhili miradi yenye kugusa vipaumbele vya serikali kwa wakati huo, pia miradi ambayo itanufaisha taasisi za serikali.
- Stakeholders’ Needs Reason: Sababu hii imejengwa na dhana ya kwamba; kampuni imezungukwa na wadau mbalimbali wenye kutofautiana mahitaji na vipaumbele. Wadau hawa ni wafanyakazi, wateja, makundi ya kijamii, mamlaka za serikali n.k. Hivyo ili kuongoza kampuni kikamilifu na kiufasaha ni lazima kuzingatia na kukidhi mahitaji na vipaumbele vya wadau hawa. Kampuni zinazochangia mashirika ya hisani kwa sababu hii, wanafadhili miradi itakayofaidisha kila kundi la wadau, mfano mradi utakaonufaisha wateja wa kampuni, wafanyakazi wa kampuni. Kampuni hizi pia zinachangia miradi inayonufaisha jamii kiujumla n.k.
Article By;
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: msongatheconsultant@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: msongatheconsultant@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA