Kwanini Kanda ya Ziwa walio CCM ndio wanawatetea sana Halima Mdee na wenzake?

Kwanini Kanda ya Ziwa walio CCM ndio wanawatetea sana Halima Mdee na wenzake?

Kea sasa watetezi wakubwa wa akina Halima Mdee na wenzake ni wanaccm kutoka Kanda ya Ziwa.

Bado sijaelewa ni kwanini!!!
Sababu ni ndogo tuu, sisi watu wa Kanda ya Ziwa ni wapenda haki na watenda haki.

Najitolea mfano mimi mwenyewe, japo sio Chadema, lakini naumia sana kila mara Chadema inapowatimua wanachama wake kinyume cha katiba sheria taratibu na kanuni.

Katiba ya Chadema iko wazi kabisa kuhusu mchakato wa vikao vya mamlaka za nidhamu. Utaratibu ni
  1. Mtuhumiwa kuandikiwa barua rasmi ya mashitaka yenye kuonyesha specific tuhuma. Hili halikufanyika, nimeuliza humu sababu hakuna anayejibu. Hii ni kinyume cha katiba ya Chadema.
  2. Barua hiyo ya mashitaka inatakiwa kukabidhiwa kwa despatch ili kuuthibisha imemfikia mhusika. Hili halikufanyika!. Ni kinyume cha katiba ya Chadema.
  3. Baada ya mtuhumiwa kupokea barua ya mashitaka, anapewa siku 14 tangu baada ya kupokea barua ya mashitaka na kuandika barua ya majibu ya tuhuma kwa maandishi. Hili halikufanyika!. Why?. Ni kinyume cha katiba ya Chadema.
  4. Baada ya siku 14, ndipo kikao cha mamlaka yake ya nidhamu kinaitishwa na kwanza kusoma majibu ya utetezi, na ndipo kikao humuita mtuhumiwa kujitetea. Hii ni moja ya misingi mikuu ya haki Duniani, "no one is condemned unheard", hakuna anayehukumiwa bila kusikilizwa!. Hili halikufanyika!. Ni kinyume cha katiba ya Chadema, ni kinyume cha katiba ya nchi, ni kinyume cha haki za binadamu!.
  5. Kikao cha CC ya Chadema, kuwaadhibu hakikufuata utaratibu huo hivyo kilikaa kama a Kangaroo Court na kuwatimua Kikangroo!.
  6. Halima Mdee ni Mwenyekiti wa Bawacha. Mamlaka ya CC ya Chadema, mwisho wa uwezo wake ni kumsimamisha tuu. Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka ya rufaa ni Mkutano Mkuu. CC ya Chadema, ilipata wapi mamlaka kumtimua Mdee?.
  7. Swali la Kwanza, Jee Kikao cha CC ya Chadema Kilichowatimua Kina Mdee ni Kikao Halali au Kilikuwa a Kangaroo Court?.
  8. Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.

    6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
    6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
    6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
    (a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
    (b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
    (c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
    (d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
    6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
    6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
    6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
    6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
    6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
    6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
    6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
    6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.

    Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
    • Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?. Huu sio Ukangaroo?
    • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?, Huu sio Ukangaroo?
    • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?. Huu sio Ukangaroo?.
    • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi cha CC kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?. Jee huu sio Ukangaroo?.
    • Jibu la Jumla ni Kikao cha CC ya Chadema, kiliwatimua wabunge wale ni a Kangaroo Court.
    • Furthermore, kweli CC ya Chadema ni mamlaka ya nidhamu kwa wabunge waChadema, sheria, taratibu na kanuni zingefuatwa, ingekuwa na mamlaka ya kuwavua uanachama wabunge hao kihalali, lakini CC ya Chadema, sio mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, CC hiyo ilipata wapi mamlaka ya kumvua uanachama Mwenyekiti wa Bawacha wakati mamlala yake ya nidhamu ni Baraza Kuu?. Huu ni ukangaroo mkubwa zaidi!
  9. Jee a Kangaroo Court moja, inapotoa hukumu Kikangaroo, kisha kikao cha rufaa, likaitishwa kuijadili ule ukangaroo wa kile kikao cha kwanza cha Kikangaroo, na kikao hiki ambacho uamuzi wake ni wa mwisho, final and conclusive, kikayabariki maamuzi yale ya Kikangaroo, ya kikao cha Kikangaroo, Je nacho kitahesabika ni kikao cha Kikangaroo au ni kikao halali, Ila maamuzi ndio ya Kingaroo, jee sasa maamuzi ya vikao vyote viwili ni maamuzi ya Kikangaroo?.


  10. Makamanda 19, kamwe msikubali ukangaroo wa aina hii kuendeshwa katika ardhi ya Tanzania!.

    A Way Forward
    Kwa vile uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu ndio final and conclusive, hakuna ubishi kuwa kina Mdee wameonewa, following precedence ya kesi Zitto Kabwe kupinga maamuzi batili kama hayo mahakaman, nawashauri kina Mdee na kundi lake, kukubali matokeo, kufungasha virago vyao kupisha, na kuiachia karma ndio iwalipie.

    Nawashauri wasiende mahakamani kutafuta haki, unless kama ni kutetea tuu ugali wao kwa kuendelea kuvuta muda wa ubunge wao ili waendelee kuvuta kwa lengo tuu ya ku service ule mkopo wa bond ya miaka 5.

    Kwa wale waumini wa karma, lets just sit and watch jinsi karma inavyofanya kazi. Kwa vile sio watu wamejaaliwa jicho la kuona the karma operatives, akina sisi wenye jicho hilo, tutakuwa tunawamegea tits and bits.

    Kunapotokea jambo kubwa kama hili, usually huwa it's not over until it's over, kwa hapa hili lilipofikia,
    it's over!.

    Paskali.
    Rejea
    Tuliuliza Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
    Tulishauri CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
    Tukaeleza Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
    Tukaonya Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
 
Ni kweli siku hizi JF tunajadiri mada yoyote tu hata Kama inawatuhumu watu bila ushahidi,hata Kama Ni wazi inaonekana mtu katunga tu Mambo yake binafsi

Ila kwa hii mada yako,umezidisha zaidi kutudharau wanna jf
Inawezeka huyo johnthebaptist analipwa "per thread", ndio maana kwa siku hazipungui nyuzi 10 anazoanzisha,na 9 kati ya hizo hazina mbele wala nyuma.
 
Back
Top Bottom