Kwanini Kanisa limejengwa katikati ya madarasa?

Chikenpox

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2022
Posts
784
Reaction score
1,246
Mimi leo nimesali Pugu Catholich church na ni parokia. Kuna kitu kimenishtua kukuta kanisa liko katikati ya madarasa ambapo kelele na fujo zote wanafunzi wanazipata moja kwa moja.

Hivi ilikuwaje Serikali ikakubali kanisa lijengwe katikati ya madarasa tena ni parokia. Je, na makanisa mengine yakitaka kujenga katikati ya madarasa hayo itakuwaje?

Serikali liangalieni hilo plz.
 
kanisa liko katikati ya madarasa
Hebu weka vizuri habari yako tukuelewe siyo wote tunaishi huko Pugu. Liko katikati ya madarasa ya nn? Madarasa yanamilikiwa na nani?

Ulikusudia kusema nn?
 
Mkuu wewe naona una uelewa mdogo sana wa mambo.Hata namna ulivyo andika hukueleza vizuri hivyo kuwafanya wasomaji wasikuelewe. Kama eneo unalozungumzia ni Pugu sekondari basi elewa kuwa hiyo shule ilikuwa ni milki ya kanisa Katoliki. Baadae ilitaifishwa na serikali lakini serikali haikutaifisha kanisa hivyo wakatoliki Bado wanalimiliki na kutumia kanisa hilo. Na Kwa nyongeza tu ni kuwa shule zote za sekondari za serikali zilikuwa za wakatoliki Zina makanisa ambayo serikali iliwaachia wenyewe Kwani lengo la serikali ilikuwa ni majengo mengine ili wanafunzi wa dini zote waweze kusomwa hapo.
 
Wewe ulikuwa kanisani kama unavyosema kelele uliziona zinatoka upande upi. Na kwa kweli kelele zinaonwa? Jumapili wanafuzi hawawi darasani. Kwa kawaida wakatoliki hawasali kwa kupiga kelele.
Kwa taarifa yako hiyo shule ilikuwa ya Katoliki na kanisa liko mahala sahihi.
Siku nyingine jifunze kuandika vizuri.
Kelele hazionwi.
 
Kiukweli uzi umeandika wewe ila aibu nimeona mimi. Ila sio mbaya hivyo vipele vya tete kuwanga huwa vinawasha sana hasa msimu huu wa Jua kali jambo ambalo limekupelekea kukosa umakini kwenye mambo ya msingi.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
 
Hii mada ni nzito na ngumu usirudie tena kujieleza hivi
 
Uwe unasoma historia
 
Sio shule zote zilikuwa za Catholic ndugu mkupuo .
Mazengo Complex ilikuwa ni ya Anglican.
Msalato Girls ilikuwa ni Anglican.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…