Kwanini Kanisa limejengwa katikati ya madarasa?

Kwanini Kanisa limejengwa katikati ya madarasa?

Mimi nilikuwa nakaa huku mjini; AZIMIO. Mapinuzi fujo sana huko; wavuta bangi walikuwepo wengi huko
Vile vile ilikuwa ni rahisi kumuona CHALWE akiwa anatoka nyumbani ili uweze ku-take cover kirahisi,,, PUGU
Ulikuwa unakosa uhundoo mapinduzi ndo ilikuwa ya maborn town boss yani kila unyama kule ulikuwepo hata msakoo walikuwa wanajishauri kuja kusachi kulee ni pa motoo,,,,daaah!pugu mabeganii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi leo nimesali Pugu Catholich church na ni parokia. Kuna kitu kimenishtua kukuta kanisa liko katikati ya madarasa ambapo kelele na fujo zote wanafunzi wanazipata moja kwa moja.

Hivi ilikuwaje Serikali ikakubali kanisa lijengwe katikati ya madarasa tena ni parokia. Je, na makanisa mengine yakitaka kujenga katikati ya madarasa hayo itakuwaje?

Serikali liangalieni hilo plz.
Wengine kabla ya kuandika uzi pateni kwanza ushauri toka kwa wenye akili..!! Jua kwanza historia ya eneo husika..!! Jua nani anamiliki nini kwenye eneo hilo..!!
 
Mleta mada ana kawaida ya kukurupuka kama uharo ndio maana huwa haeleweki na huwa anaandika viti visivyo na miguu wala kichwa!
 
Kwanini usingeenda kumuuliza baba Paroko unataka serikali iangalie nini ulienda kusali au tambua serikali ilichukua shule nyingi sana za kanisa Nenda Umbwe, wamisionari wa kikatoliki sera yao ilikua Mungu, elimu na afya ndio maana utakuta Zahanati, kanisa na Shule.

Sidhani kama wewe ni Mkatoliki tafuta kitabu cha miaka 100 ya umisionari Tanzania ujisomee utapata cha kujifunza.
Aende Paramiho, Ndanda, Kigonsera etc akaone. Asijilalamishe tu hapa
 
Mimi leo nimesali Pugu Catholich church na ni parokia. Kuna kitu kimenishtua kukuta kanisa liko katikati ya madarasa ambapo kelele na fujo zote wanafunzi wanazipata moja kwa moja.

Hivi ilikuwaje Serikali ikakubali kanisa lijengwe katikati ya madarasa tena ni parokia. Je, na makanisa mengine yakitaka kujenga katikati ya madarasa hayo itakuwaje?

Serikali liangalieni hilo plz.
Shule ilikuwa ya kanisa, walijenga wenyewe wamisionari, hawakutegema kama iko siku serikali itaitaifisha. Hivyo hiyo serikali unayotaka iliangalie hilo suala, haina cha kufanya, pengine ni kuhakikisha shughuli za kanisa haziingiliani na shughuli za ufundishaji, kama unavyodai kelele.
 
Back
Top Bottom